DKT. MWAMBA AFANYA MAZUNGUMZO NA MKURUGENZI WA AFD AFRIKA MASHARIKI

Shirika la la Maendeleo la Ufaransa (AFD) limeahidi kuendelea kushirikiana na Tanzania katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ya nishati mabadiliko ya tabia nchi, maji, uchumi wa buluu, kilimo na sekta ya usafirishaji. Ahadi hiyo imetolewa jijini Dodoma wakati wa Mkutano wa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba na Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika Mashariki wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD), Bw. Jean Francois Arnal, uliojadili kuhusu ushirikiano wa maendeeo kati ya Tanzania na Ufaransa.