DKT. MWAMBA AFANYA MAZUNGUMZO NA AFISA MTENDAJI MKUU WA TAASISI YA BWB YA UINGEREZA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, amekutana na kufanya mazungumzo na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Bankers Without Boundaries (BWB) kutoka Uingereza, Bw. Chris Smith, ambapo wamejadili masuala ya ushirikiano wa kimaendeleo katika sekta mbalimbali zikiwemo Afya, elimu, Uchumi na maendeleo ya kijamii. Mazungumzo hayo ambayo yamefanyika jijini Dodoma yamehudhuriwa na Kamishna wa Idara ya Usimamizi wa Madeni, Bw. Japhet Justin, Mkurugenzi wa Taasisi ya BWB, Bw. Matteo Scalabrino na wajumbe wengine kutoka pande hizo mbili.