DKT. MPANGO AFUNGUA MKUTANO WA MAENDELEO YA RASILIMALI WATU
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, amefungua mkutano ngazi ya Mawaziri, kuelekea Mkutano wa Wakuu wa nchi 54 za Afrika kuhusu masuala ya Maendeleo ya Rasilimali Watu (Africa Heads of State Human Capital Development Summit), utakaofanyika julai 26, 2023, katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam.