BILIONI 96.5 KUONGEZA KASI YA MRADI WA UMEME WA KAKONO

Serikali ya Tanzania na Shirika la Maendeleo la Ufaransa zimesaini mkataba wa Euro milioni 34.86 sawa na takribani shilingi bilioni 96.47 kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa mtambo wa kufua umeme wa Kakono. Mkataba huo umesainiwa jijini Dodoma na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba na Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa nchini Tanzania, Bi. Celine Robert.