BI. OMOLO APONGEZA WIZARA YA FEDHA NA TAASISI ZAKE KWA UTOAJI WA ELIMU MAONESHO YA NANENANE DODOMA.
Naibu Katibu Mkuu anayesimamia masuala ya Huduma za Hazina, Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo, ametembelea Banda la Wizara ya Fedha kwenye Maonesho ya Nanenane yanayofanyika Kitaifa katika Viwanja vya Nanenane, Nzuguni Jijini Dodoma ili kujionea huduma zinazotolewa na Wizara pamoja na Taasisi zake.
Bi. Omolo ameipongeza Wizara na Taasisi kwa kushiriki katika Maonesho hayo yaliyokuwa na kauli mbiu “ChaguaViongozi Bora kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo na Uvuvi2025’’, ili kufikisha elimu kwa wananchi hasa katika sekta ya kilimo ili kuchochea ukuaji wa sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi.