BENKI YA DUNIA YARIDHISHWA MA MAENDELEO YA TANZANIA YAIPATIA DOLA MILIONI 550

Benki ya Dunia, Kupitia Bodi yake ya Wakurugenzi, imeiidhinishia Tanzania dola za Marekani milioni 550 sawa na zaidi ya shilingi trilioni 1.4 kwa ajili ya kutekeleza miradi miwili ya kimkakati katika sekta za elimu na kusaidia kaya masikini. Uamuzi huo wa Benki umetangazwa na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayesimamia Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini, Dkt. Ndiame Diop, alipokutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar, pembezoni mwa Mikutano ya Majira ya Kipupwe ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa IMF, Makao Makuu wa Taasisi hizo Jijini Washington D.C, nchini Marekani.