BENKI YA DUNIA YAIDHINISHIA TANZANIA MKOPO NAFUU WA SHILINGI TRILIONI 5

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, ameishukuru Benki ya Dunia kwa kuitengea Tanzania jumla ya dola za Marekani bilioni 2.1 sawa na shilingi trilioni 4.9 katika mzunguko wa 20 wa IDA (Julai 2022 – Juni 2025) kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotarajiwa kuchochea ukuaji wa uchumi wa nchi pamoja na kupunguza umasikini wa watu wake.