BENKI YA DUNIA YAFADHILI MPANGO WA TAKWIMU TANZANIA
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, amesema kuwa Mfumo wa Kitaifa wa Takwimu unaofanya kazi kwa ufanisi, gharama nafuu na wenye uwezo wa kutoa takwimu bora na za uhakika utasaidia nchi kuweka mipango yake ya maendeleo ikiwa ni pamoja na kufanya tathmini ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano, wa mwaka 2020 - 2025 na maandalizi ya Mpango wa Maendeleo wa 2025 - 2030.
Dkt. Mwamba amesema hayo wakati akifungua kikao cha kwanza cha Kamati ya Uongozi ya Pamoja ya Awamu ya Pili ya Mpango Kabambe wa Kuboresha na Kuimarisha Takwimu nchini, yaani Tanzania Statistical Master Plan II, Jijini Dar es Salaam.