BENKI YA DUNIA KUSHIRIKIANA NA TANZANIA KUTEKELEZA PPP

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Lawrence Mafuru amesema kuwa Serikali inafanya majadiliano ya kimkakati na Benki ya Dunia (WB) namna ya kuiwezesha sekta binafsi kushiriki katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo kupitia mpango wa ushirikiano kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi, yaani PPP.