BENKI YA DUNIA KUISAIDIA TANZANIA UTEKELEZAJI WA MIRADI 14 YA KIMKAKATI
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (kushoto), akiwa katika picha na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia, anayesimamia nchi za Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika, Bi. Victoria Kwakwa, mara baada ya kumalizika kwa kikao chao, katika Ofisi za Makao Makuu ya Benki hiyo, jijini Washington D.C, nchini Marekani, wakati wa mikutano ya Majira ya Kipupwe (Spring Meetings) ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) yenye kauli mbiu ya “Vision to Impact” inayoendelea jijini humo.