BALOZI OMAR: MAGEUZI YA UCHUMI KUCHANGIA USTAWI WA WANANCHI

Waziri wa Fedha Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), amesema kuwa mageuzi ya uchumi yataendelea kuwa ajenda ya muda mrefu yakilenga si tu kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi bali kuhakikisha ukuaji huo unachangia katika upatikanaji wa ajira na ustawi wa wananachi kwa ujumla. Amebainisha hayo wakati wa kikao na Timu ya Wataalamu kutoka Taasisi ya kimataifa inayojihusisha na tathmini ya nchi kukopesheka katika masoko ya mitaji ya kimataifa ya Moody’s Investor Service ikiongozwa na Bw. John Walsh, kilichofanyika Ofisi za Treasury Square, jijini Dodoma.