AfDB YAIPATIA TANZANIA MKOPO NA MSAADA KWA AJILI YA KUENDELEZA KILIMO
Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imeipatia Tanzania mkopo wenye mashariki nafuu pamoja na msaada wenye thamani ya dola za Marekani milioni 75.5, sawa na shilingi bilioni 175 za kitanzania kwa ajili ya kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula nchini kupitia mradi wa upatikanaji wa pembejeo za kilimo.