AfDB YAAHIDI KUENDELEZA USHIRIKIANO NA TANZANIA KUKUZA UCHUMI

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) anayeshughulikia Nishati, Dkt. Kevin Kariuki, ambapo ameishukuru Benki hiyo kwa kufadhili miradi 29 ya kitaifa na kikanda, yenye thamani ya zaidi ya dola za kimarekani bilioni 3.84 Dkt. Nchemba amesema jijini Dodoma kuwa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imekuwa mdau mkubwa wa maendeleo ambapo kati ya miradi hiyo, miradi 26 ni ya kitaifa na 3 ni ya kikanda ambayo iko katika sekta za miundombinu ya barabara, nishati, maji na kilimo.