Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

WIZARA YA FEDHA YATOA MAFUNZO KWA WAZABUNI KUTOKA BOTSWANA

15 Mar, 2023
WIZARA YA FEDHA YATOA MAFUNZO KWA WAZABUNI KUTOKA BOTSWANA

Mwenyekiti wa Ujumbe wa Wataalam kutoka Mamlaka ya Rufaa za Zabuni ya Ununuzi wa Umma nchini Botswana, Mhe. Jaji Lebotse Kenneth, akipeana mkono na Kaimu Mwenyekiti wa Mamlaka ya Rufaa ya Zabuni za Umma -PPAA Wakili Rosan Mbwambo, walipowasili kwenye Ofisi za Mamlaka ya Zabuni ya Ununuzi wa Umma Tanzania (PPAA) jijini Dodoma.

 

Wataalamu kutoka Mamlaka ya Rufaa ya Zabuni ya Ununuzi wa Umma nchini Botswana wameipongeza Tanzania kwa kuwa na mifumo imara ya ununuzi na utatuaji wa migogoro ya ununuzi hatua inayochangia kupata wazabuni na wakandarasi wernye sifa za kutekeleza miradi ya maendeleo.

Hayo yameelezwa jijini Dodoma na Msajili wa Mamlaka ya Zabuni ya Ununuzi wa Umma nchini Botswana, Bw. Geoffrey Gotshega, akiongoza ujumbe walipofanya ziara ya mafunzo Wizara ya Fedha na Mipango kujifunza mambo mbalimbali kuhusu utekelezaji wa sera za ununuzi.

Bw. Gotshega alisema kuwa Mamlaka ya Zabuni ya Ununuzi wa Umma Botswana ni mpya, hivyo wamekuja kujifunza namna ya mfumo wa ununuzi Tanzania ulivyoundwa na unavyofanyakazi.

“Mifumo ya ununuzi ya Tanzania ni madhubuti kwa kuwa kanuni zake ni imara, ununuzi unafanyika kwa uwazi kwa njia ya kielektroniki na malalamiko yanafanyiwa kazi kwa uharaka na kuwezesha miradi kufanyika kwa wakati na kuipunguzia serikali gharama”, alisema Bw.Gotshega .

Akielezea kuhusu ziara hiyo Kamishna Msaidizi wa Idara ya Sera ya Ununuzi wa Umma wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Alex Haraba, alisema kuwa amewaeleza kuhusu Sera ya ununuzi wa umma inayosimamiwa hiyo na majukumu yake ikiwa ni pamoja na kusimamia, kutekeleza na kushughulikia malalamiko ya ununuzi wa umma ili kuwa na tija katika ununuzi wa umma kwa mwananchi na Taifa kwa ujumla.

Kwa upande wake, Katibu Mtendaji wa Mamlaka ya Rufaa ya Zabuni za Umma -PPAA, Bw. James Sando, alisema lengo la wataalam hao wa sekta ya uzabuni kuja Tanzania ni kutaka kujifunza na kuangalia jinsi ambavyo Tanzania inafanya kazi ya ununuzi na namna itakavyowasaidia katika utendaji kazi wao kwa sababu wamepitisha sheria yao ya ununuzi hivi karibuni.

“Tanzania tumeanza kutekeleza Sheria ya ununuzi miaka 23 iliyopita na tumekuwa na Mamlaka ya Rufaa, ndio maana wenzetu wamekuja kuangalia namna tunavyoendesha mashauri katika Mamlaka na wamefurahia ujuzi tuliowapa”, alisema Bw. Sando.

Bw. Sando aliongeza kuwa pamoja na utekelezaji wa majukumu yao PPAA pia wanashughulikia mashauri ambayo yanatokea katika ununuzi wa umma nchini.

Alisema kuwa mteja aliyeomba zabuni na ana malalamiko ambayo yameanzia mchakato katika ununuzi anaweza kwenda PPAA baada ya kuwa amewasilisha kwa Afisa Masuuli na kama Afisa Masuuli atakuwa ametoa maamuzi ndani ya siku saba na hajaridhika anaweza kwenda kwenye Mamlaka hiyo.

Alieleza kuwa, hata kama mchakato mzima wa ununuzi umekamilika na tuzo imetolewa na mradi umeanza kufanyiwa kazi na mikataba ilisainiwa, Mamlaka inaweza kusikiliza lalamiko  na kutoa ufumbuzi.

Ujumbe huo kutoka Botswana unaendelea na ziara hiyo ya mafunzo ambapo wajumbe hao wametembelea Wizara ya Fedha na Mipango na Mamlaka ya Rufaa ya Zabuni za Umma -PPAA, jijini Dodoma.  

Mwisho.