Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2024/2025
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

WIZARA YA FEDHA YAENDELEA NA UCHAMBUZI WA BAJETI SEKTA YA UZALISHAJI

18 Mar, 2026
WIZARA YA FEDHA YAENDELEA NA UCHAMBUZI WA BAJETI SEKTA YA UZALISHAJI

Kamishna Msaidizi wa Idara ya Usimamizi wa Bajeti ya Serikali, Bw. Fundi Makama, akiongoza kikao kazi cha wataalamu wa Wizara, Idara Zinazojitegemea, Wakala za Serikali, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa cha kupitia, kuchambua na kujadili mipango na mapendekezo ya bajeti yaliyowasilishwa na Sekta ya Uzalishaji ikiwemo, Wizara ya Kilimo, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Ardhi, Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na Wizara ya Madini ili kuhakikisha kuwa yanazingatia vipaumbele na Mipango ya Taifa, sera na mikakati ya maendeleo, pamoja na miongozo ya upangaji na uandaaji wa bajeti, kikao hicho kinafanyika katika Ukumbi wa Kambarage, Wizara ya Fedha, (Treasury Square) jijini Dodoma.

 

Wizara ya Fedha kupitia Idara ya Usimamizi wa Bajeti ya Serikali, inaendelea na uchambuzi wa bajeti ya sekta ya uzalishaji kwa mwaka wa fedha 2026/2027. Sekta hiyo inajumuisha Wizara ya Kilimo, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Ardhi, Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na Wizara ya Madini.

Hatua hiyo inalenga kuchambua na kujadili mipango na mapendekezo ya bajeti ya sekta muhimu za uzalishaji ili kuhakikisha yanazingatia vipaumbele vya Taifa, sera za maendeleo, mikakati ya kitaifa pamoja na miongozo ya upangaji na uandaaji wa bajeti.

Kikao hicho kimeongozwa na Kamishna Msaidizi wa Idara ya Usimamizi wa Bajeti ya Serikali, Bw. Fundi Makama na kuhudhuriwa na Wakurugenzi wa Sera na Mipango pamoja na wataalamu kutoka wizara na sekta husika. 

Kikao hicho kimefanyika katika Ukumbi wa Kambarage, Treasury Square, jijini Dodoma ambapo, washiriki walipata nafasi ya kujadili kwa kina namna bajeti za sekta za uzalishaji zinavyoweza kuyafikia malengo yaliyowekwa kwenye Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 na kuimarisha uchumi wa Taifa na kuchochea maendeleo endelevu.

Mwisho.