Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2024/2025
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

WIZARA YA FEDHA YAENDELEA KUPONGEZWA KWA WELEDI WA UTOAJI ELIMU

22 Jun, 2025
WIZARA YA FEDHA YAENDELEA KUPONGEZWA KWA WELEDI WA UTOAJI ELIMU

Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu (Mb) (kulia) akisalimiana na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dunstan Kitandula (Mb), baada ya kutembelea Banda la Wizara ya Fedha, kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, viwanja vya Chinangali, jijini Dodoma.

 

Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu (Mb) ameipongeza Wizara ya Fedha kwa kushiriki kikamilifu katika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa kutoa elimu kwa weledi kwa wananchi.

Pongezi hizo amezitoa alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha, katika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika Viwanja vya Chinangali, jijini Dodoma kuanzia Juni 16 hadi 23 mwaka huu.

Amesema kuwa elimu kuhusu masuala ya Bajeti, Usimamizi wa Mali za Serikali, , Usimamizi wa Deni la Taifa, Mifumo ya Fedha na Pensheni inayotolewa na Hazina kwa Wastaafu ni muhimu kwa wananchi wote wakiwemo watumishi wa umma.

Pongezi hizo zimetolewa baada ya kupata maelezo ya huduma zinazotolewa katika Wiki ya Utumishi wa Umma na Afisa Mwandamizi wa Idara ya Usimamizi wa Deni la Taifa, Bw. Sepo Seni.

Kwa upande mwingine, Afisa Mwandamizi wa Idara ya Mhasibu Mkuu wa Serikali, Bi. Stellah Mtally, amewataka wakazi wa Dodoma na maeneo mengine nchini kufahamu kuwa Ofisi ya Pensheni Hazina inajukumu la kulipa mafao ya kustaafu kwa viongozi wa kitaaifa na kisiasa na watumishi wa umma ambao hawachangii katika mifuko ya hifadhi ya jamii.

Bw. Mtally aliyasema hayo wakati akitoa elimu ya pesheni inayolipwa na Hazina kwa wastaafu kwa watu waliotembelea Banda la Wizara ya Fedha katika Maadhimisho hayo

Alisema kuwa aina za Mafao yanayotolewa na Ofisi ya Pensheni Hazina ni pamoja na Mafao ya Kiinua Mgongo yanayolipwa kwa mkupuo mmoja kwa mtumishi anapostaafu kwa mujibu wa Sheria.

Alitaja mafao mengine kuwa ni pamoja na Pensheni ya kila Mwezi anayolipwa mstaafu baada ya kustaafu, Mafao ya Mirathi, Pensheni ya Kifo, Mafao kwa Wategemezi wa marehemu ambaye alikuwa kwenye ajira ya masharti ya kudumu na malipo ya uzeeni, ambapo marehemu anatakiwa kuwa alifanya kazi muda usiopupungua miaka 15.

Aidha Bi. Mtally alisema pia kuna mafao ya pensheni ya ulemavu na mafao ya mkataba ambayo ndiyo kiinua mgongo.

Mwisho.