Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2024/2025
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

WATAALAMU WA UNUNUZI NA UGAVI WATAKIWA KUONGEZA BIDII

20 Dec, 2024
WATAALAMU WA UNUNUZI NA UGAVI WATAKIWA KUONGEZA BIDII
Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Bw. Missaile Musa, (katikati), akitembelea mabanda mbalimbali ya Maonesho kabla ya kufunga Kongamano la 15 la Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi kwa niaba ya Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb).
 
Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi nchini wametakiwa kufanya kazi kwa bidii na weledi ili kuleta maendeleo ya wananchi kwakuwa ndiyo dhamira ya Serikali. 
Hayo yalisemwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Bw. Missaile Musa, wakati akifunga Kongamano la 15 la Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi kwa niaba ya Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano (AICC) Jijini Arusha.

Aliongeza kuwa eneo la ununuzi na ugavi ni eneo muhimu katika utendaji wa taasisi nyingine ikiwemo taasisi za Serikali, hivyo wataalamu hao wanapaswa kutekeleza wajibu wao na kuondosha vikwazo mbalimbali katika ununuzi na ugavi.

‘’Niwaombe wataalamu, twendeni katika maeneo yetu ya kazi, tukatimize majukumu yetu kwa weledi zaidi kwa kuondoa changamoto zote zilizojadiliwa hapa ili kuendelea kulisukuma gurudumu la maendeleo ya nchi yetu’’alisema Bw. Musa
 
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya  Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) Bw. Benezeth Ruta, alisema kuwa washiriki walijadili masuala mbalimbali muhimu kwa ajili ya kuendelea kuboresha huduma za ununuzi na ugavi ili kuendana na mazingira ya sasa.
 
‘’Kongamano la mwaka huu, lilijielekeza kujadili Mabadiliko ya kidigitali katika kuboresha usimamizi wa mnyororo wa ununuzi na ugavi kwa maendeleo endelevu’’ alisema Bw. Ruta.
 
Bw. Ruta aliongeza kuwa wataalam hao wa Ugavi na Ununuzi wamepata nafasi ya kujadili mada zote zilizowasilishwa na wamepata kupanua mawazo juu ya mchango wa fani hiyo katika kukuza uchumi wa viwanda katika nchi yetu.
Kongamano la Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi ambalo lilikuwa na kauli mbiu ya 
 
“Mabadiliko ya Ununuzi na Ugavi kwa Usimamizi Bora wa Rasilimali”, linafanyika kila mwaka ambapo zaidi ya washiriki 1,800 wamehudhuria Kongamano la mwaka huu huku washiriki wakiongezeka ukilinganisha na mwaka jana.
 
Mwisho.