Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2024/2025
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

WATAALAMU WA UBIA TANZANIA BARA NA ZANZIBAR WAJADILI UBIA

05 Feb, 2026
WATAALAMU WA UBIA TANZANIA BARA NA ZANZIBAR WAJADILI UBIA

Mkurugenzi wa Idara ya Mipango, Sera na Utafiti, Wizara ya Kazi na Uwekezaji- Zanzibar, Bi. Bihindi Nassor (Katikati, mstari wa mbele), akiwa katika picha ya pamoja na Mchumi Mkuu kutoka Kitengo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPU), Wizara ya Fedha, Bi. Josephina Melkiol Buhili (watatu kushoto), Afisa Mwandamizi Msimamizi wa Fedha, Idara ya Maandalizi na Uchambuzi wa Miradi kutoka Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPC), Bi. Mwanaidi Araba, Mchumi kutoka Kitengo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPU), Wizara ya Fedha, Bi. Anastazia Amandi (wa kwanza kulia) pamoja na wataalamu wengine wa masuala ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP) mara baada ya kikao cha wataalamu hao katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha jijini Dar Es Salaam.

 

Wataalamu kutoka Kitengo cha Ubia Kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP), Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPC), na Wataalam kutoka Wizara ya Kazi na Uwekezaji, Zanzibar, kupitia Idara ya Mashirikiano kati  ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPD), wamekutana na kujadili kuhusu maandalizi ya Kikao cha Kwanza cha Ushirikiano  kati ya pande zote mbili kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar Es Salaam.

Katika kikao hicho wataalamu hao walijadili masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupitia na kuthibitisha ajenda zitakazojadiliwa katika Kikao cha Kwanza cha Ushirikiano huo.

Wataalamu hao pia walipitia taarifa ya utekelezaji wa yatokanayo na kikao cha pili cha Ushirikiano kwa mwaka wa fedha 2024/2025, na kupata wasilisho kuhusu Rasimu ya Mwongozo wa Usimamizi wa Misaada ya Kibajeti na Madeni Sanjari.