Category Title

 • Government Budget Speeches
 • Ministry's Budget Speeches
 • Budget Books 2024/2025
 • Budget Books 2023/2024
 • Budget Books 2022/2023
 • Budget Books 2021/2022
 • Budget Books 2020
 • Budget Books 2018/2019
 • Budget Books 2015/2016
 • Budget Books 2014/2015
 • Content not found
 • Content not found
 • Content not found

WASTAAFU WAASWA KUWA MAKINI NA MATAPELI

13 Jun, 2024
WASTAAFU WAASWA KUWA MAKINI NA MATAPELI

Afisa Mkuu Mwandamizi Idara ya Uendeshaji wa Sekta ya Fedha, Bw. Salim Kimaro akitoa elimu ya kujipanga kuhusu maisha ya kustaafu iliyofanyika katika Ukumbi wa Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo Mkoa wa Rukwa.

 

Serikali imewaasa Wastaafu na Wastaafu watarajiwa kuwa makini na matapeli, kuanzisha biashara wasizokuwa na uzoefu nazo pamoja na kuepuka washauri wasiokuwa na nia nzuri ambao wanataka kujinufaisha wao wenyewe.

Afisa Mkuu Mwandamizi Idara ya Uendeshaji wa Sekta ya Fedha, Bw. Salim Kimaro aliyasema hayo alipokuwa akitoa semina ya Elimu ya Fedha kwa wanavikundi na wajasiriamali wadogo katika ukumbi wa Ofisi za Halmashauri Wilaya ya Kalambo Mkoa wa Rukwa.

Bw. Kimaro alisema kumekuwa na wimbi la matapeli wanaotoa ushauri usiofaa kwa wastaafu na pia kwa wale walioko kwenye mifuko ya kijamii wamekuwa wakitapeliwa kwa kupigiwa simu huku wakiomba fedha na kuwaahidi kuwa watawasaidia walipwe mafao yao haraka.

“Kumekuwa na wimbi la matapeli wanatoa ushauri usiofaa kwa wastaafu kwa kuwa wanafahamu sasa wamepata hela nyingi za kiinua mgongo, kwa hiyo kila mmoja anakwenda kumshauri lakini ushauri ule unakuwa kwa ajili ya kuwanufaisha wao wenyewe. Hivyo tunatoa rai wastaafu wawe makini sana na ushauri wanaopewa na hawa watu ili wasiingie kwenye hii kadhia ya kutapeliwa na endapo itatokea ukapigiwa simu ya kudai chochote ili upate mafao yako kwa wakati au kwa haraka tafadhali toa taarifa kwa Mfuko wowote wa Hfadhi ya Jamii uliopo ili suala hilo lifuatiliwe na kuchukuliwa sheria”. Alisema Bw. Kimaro.

Aidha, Bw.Kimaro, aliwashauri wastaafu na wastaafu watarajiwa kuwa wanapaswa kujiandaa kustaafu pindi wanapopata ajira au siku ya kuanza kupata kipato kwa kuwa na tabia ya kujiwekea akiba kwenye taasisi, vikundi au SACCOS zilizosajiliwa kwa ajili ya maisha ya baadae.

Serikali inaendelea kutoa elimu kwa umma, ikiwa na lengo la kuwafikia Watanzania wote na kuwajengea uwezo wa uelewa kuhusu masuala ya fedha, kuweka akiba, uwekezaji, usimamizi wa fedha binafsi, kujipanga kuhusu Maisha ya kustaafu pamoja na masuala ya usimamizi wa sheria na kanuni za huduma ndogo za fedha.  

Mwisho