Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2024/2025
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

WANANCHI WASHAURIWA KUWA NA UTAMADUNI WA KUWEKA AKIBA YA FEDHA

13 Jun, 2024
WANANCHI WASHAURIWA KUWA NA UTAMADUNI WA KUWEKA AKIBA YA FEDHA

Afisa Usimamizi wa Fedha katika Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha - Wizara ya Fedha, Bw.Stanley Kibakaya, akitoa elimu ya fedha kwa baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha Afisa Tabibu Kibondo, mkoani Kigoma.

 

Wananchi wametakiwa kukopa mikopo yenye faida kwenye taasisi au mtu binafsi ambaye ana leseni iliyotolewa na Benki Kuu ya Tanzania ili kuwa na uhakika wa mkopo na kuondoa changamoto kwa wananchi hao.

Wito huo umetolewa katika Kata ya Mabamba, Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma na Afisa Usimamizi wa Fedha katika Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha katika Wizara ya Fedha Bw. Stanley Kibakaya, wakati wa zoezi la kutoa elimu ya fedha kwa wananchi wa makundi mbalimbali katika Mkoa wa Kigoma.

“Hakikisha unapokwenda kukopa, mkopeshaji awe na leseni kwa kuwa mtoa huduma huyo atakuwa amekidhi vigezo na masharti vilivyowekwa na mamlaka husika”, alisema Bw. Kibakaya.

Aidha, aliwahimiza wafanyabiashara kuwa na utamaduni wa kuweka akiba ili kuweza kutambua mapato wanayo yapata kupitia biashara zao

Alisema kuwa wakitunza fedha lazima wawe na malengo ili akiba hiyo iwe na faida na pia ni vema wahifadhi fedha kwenye akaunti za Benki au kwenye simu,  sehemu ambazo ni salama ili kuepuka hasara au upotevu.

Kuhusu uwekezaji, Bw. Kibakaya, alisema kuwa   jambo hilo si kwa ajili ya watu wenye kampuni kubwa pekee bali hata mwananchi wa kawaida anaweza kuwekeza kupitia biashara ndogondogo anazozifanya.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Mabamba, Wilayani Kibondo Bw. Shedrack Chongela, aliipongeza Wizara ya Fedha kwa elimu waliyoitoa kwa wananchi hao huku akiwakumbusha wananchi wanapokwenda kuchukuwa mikopo waende maeneo yenye kukidhi vigezo.

Naye Mkazi wa Kijiji cha Mabamba, Wilaya ya Kibondo, Bi. Felister Kazombe, alisema kuwa semina hiyo ni muhimu kwa jamii yao kwa kuwa imetoa mwongozo mzuri kuhusu masuala ya fedha.

Mwisho.