Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2024/2025
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

WANANCHI WAMIMINIKA KUPATA ELIMU BANDA LA WIZARA YA FEDHA- SABASABA

30 Jun, 2025
WANANCHI WAMIMINIKA KUPATA ELIMU BANDA LA WIZARA YA FEDHA- SABASABA

Afisa Mwandamizi wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bi. Mary Mihigo, akitoa elimu kuhusu utaratibu wa utoaji huduma ndogo za fedha kwa mkazi wa Dar es Salaam, Bw. Gabiriel Weslaus, aliyetembelea Banda la Wizara ya Fedha, kwenye Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Dar Es salaam (Sabasaba) ambayo yameanza  tarehe 28 Juni na kutarajiwa kuhitimishwa Julai 13 mwaka huu.

 

Wananchi wametakiwa kuhakikisha wanakopa katika maeneo rasmi ili kuondoa changamoto ya mikopo umiza ambayo imekuwa ikileta adha kwa wananchi kwa kufilisiwa mali zao.

Akizungumza katika Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Dar Es salaam (Sabasaba) Afisa Mwandamizi wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bi. Mary Mihigo  amesema Serikali imeweka utaratibu wa kujisajili kwa watoa huduma za fedha ili kukomesha tatizo hilo.

Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Dar Es salaam (Sabasaba) ambayo yameanza tarehe 28 Juni yanatarajiwa kuhitimishwa Julai 13 mwaka huu, ambapo Wizara ya Fedha na Taasisi zake zinashiriki kikamilifu kutoa huduma kwa karibu kwa wananchi kupitia Maonesho hayo.

Mwisho.