Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2024/2025
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

WANANCHI WAHIMIZWA KUPAKUA GePG APP TANZANIA KURAHISISHA MALIPO

22 Jun, 2025
WANANCHI WAHIMIZWA KUPAKUA GePG APP TANZANIA KURAHISISHA MALIPO

Kamishna Msaidizi wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha Wizara ya Fedha, Bi. Janeth Hiza, akipata maelezo kwa Afisa Mwandamizi wa Idara ya Usimamizi wa Mali za Serikali, Bw. George Kilo, kuhusu elimu ya usimamizi wa mali za Serikali unavyotolewa katika  Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, viwanja vya Chinangali, jijini Dodoma.

 

Wananchi wenye Simu janja wametakiwa kupakua Aplikesheni ya Mfumo wa Kielektroniki wa Malipo ya Serikali (GePG) ili kuwarahisishia katika ufanyaji wa malipo mbalimbali ya huduma za Serikali.

Hayo yameelezwa na Afisa Mwandamizi wa Idara ya Usimamizi wa Mifumo ya Fedha na Tehama Wizara ya Fedha, Bw. Charles Maganga, wakati akitoa elimu kwa wananchi waliotembelea Banda la Wizara ya Fedha katika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika Viwanja vya Chinangali, jijini Dodoma.

Bw. Maganga alisema kuwa Aplikesheni  ya GePG Tanzania ni programu ya simu ambayo inawezesha watumiaji kuuliza, kutathmini na kulipia ankala za Serikali kwa kupitia Simu janja ya Kiganjani (Smartphone).

Alisema Aplikesheni hiyo inarahisisha ulipaji kwa uharaka zaidi na utunzaji wa Kumbukumbu za malipo ambapo mtumiaji pia anaweza kupata taarifa za ankala (Biliş) kuhakiki mita namba, kununua Luku, kuandaa na kulipia Loss Report pamoja na kukadiria kodi ya ardhi.

Pia inaweza kutumika kulipia maegesho, kulipa faini za makosa ya barabarani na kupata ankara ya maji kwa kutumia akaunti namba na huduma nyingine za Serikali,

inamsaidia mtumiaji kuhakiki namba ya malipo, Risiti ya Benki na Risiti ya GePG.

Mwisho.