Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2024/2025
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

VIKUNDI VYA HUDUMA NDOGO ZA FEDHA VIJISAJILI WEZESHA PORTAL

13 Jun, 2024
VIKUNDI VYA HUDUMA NDOGO ZA FEDHA VIJISAJILI WEZESHA PORTAL

Afisa Uwezeshaji kutoka Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi kiuchumi, Bw. Omar Bakari, akitoa elimu ya usajili wa vikundi vya huduma ndogo za fedha iliyofanyika katika moja ya darasa la Shule ya Msingi Kipeta, Wilaya ya Sumbawanga Vijijini, mkoani Rukwa.

Serikali imewashauri wananchi kusajili vikundi vyao vya huduma ndogo za fedha kupitia mfumo wa Wezesha Portal ambayo ni njia rahisi na haina gharama yoyote. 

Ushauri huo umetolewa na Afisa Uwezeshaji kutoka Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Bw. Omar Bakari, wakati akitoa Elimu ya Huduma Ndogo za Fedha katika Kijiji cha Kipeta, Wilaya ya Sumbawanga Vijijini, Mkoani Rukwa.

Bw. Bakari alisema kuwa kabla ya kusajili vikundi vya huduma ndogo za fedha ni vyema wananchi wanaotaka kuanzisha vikundi hivyo wakajiridhisha kuhusu wanachama wao wanaotaka kujiunga nao ili kuepukana na lawama na baadhi ya wajumbe kukimbia familia zao kutokana na madeni.

“Kabla ya kujiunga kwenye kikundi kitu cha kwanza lazima wawe wanatoka eneo moja ili kurahisisha utambuzi katika Serikali za mitaa, pili lazima waaminiane, tatu wawe na lengo moja lililosababisha wao waamue kuanzisha kikundi. “Alisema Bw. Bakari

Aidha, Bw. Bakari aliwawashawishi wananchi kuendelea kusajili vikundi vyao kupitia wezesha Portal kwani inaokoa muda.

Wezesha Portal ni jukwaa la dijitali lililoundwa kusaidia wajasiriamali na wafanyabiashara katika kukuza biashara zao, kupata mafunzo, na kupata rasilimali zingine za kuwasaidia kibiashara.

Mwisho