Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2024/2025
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

UHUSIANO WA TANZANIA NA KOREA KUSINI WAZIDI KUIMARIKA

20 Feb, 2026
UHUSIANO WA TANZANIA NA KOREA KUSINI WAZIDI KUIMARIKA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-Maamry Mwamba akiagana na Balozi wa Korea Kusini nchini Tanzania, Mhe. Eunje Ahn, baada ya mkutano kati yao kuhusu ushirikiano wa maendeleo, uliofanyika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam.

 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-Maamry Mwamba, amesema kuwa Serikali ya Tanzania inatambua na kuthamini mchango mkubwa wa Korea Kusini katika sekta mbalimbali, kupitia nafasi yake kama mshirika wa maendeleo na rafiki wa karibu.

Dkt. Mwamba amesema hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Korea Kusini nchini Tanzania, Mhe. Eunje Ahn, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, Jjini Dar es Salaam, ambapo  mazungumzo hayo yalihusu namna ya kuendeleza na kuimarisha ushirikiano wa maendeleo kati ya mataifa hayo mawili. 

Aidha, aliishukuru Serikali ya Korea Kusini kwa msaada wa kifedha kupitia mikopo nafuu na ruzuku, ambazo zimekuwa chachu ya utekelezaji wa miradi ya miundombinu na maendeleo nchini.

Katika mazungumzo hayo, Dkt. Mwamba pia alitoa salamu kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akisisitiza dhamira ya Serikali ya Tanzania ya kuimarisha zaidi ushirikiano wa pande mbili kwa manufaa ya wananchi wa mataifa haya mawili.

Kwa upande wake, Balozi wa Korea Kusini nchini Tanzania Mhe. Eunje Ahn, aliahidi kuwa Serikali yake  itaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika miradi ya kimkakati, ili kuhakikisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi yanapatikana kwa manufaa ya wananchi wa mataifa hayo. 

Kikao hicho kilihudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban, Kamishna Msaidizi, Idara ya Fedha za Nje, Wizara ya Fedha Bw. Melckzedeck Mbise na mwakilishi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. 

MWISHO