Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2024/2025
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

TRADE MARK AFRIKA KUENDELEA KUTEKELEZA MIRADI NCHINI

28 Jun, 2024
TRADE MARK AFRIKA KUENDELEA KUTEKELEZA MIRADI NCHINI

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban, na Mkurugenzi Mkazi wa TradeMark Africa (TMA), Bw. Elibariki Shammy, wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe kutoka taasisi mbalimbali zinazotekeleza miradi inayofadhiliwa na TMA baada ya kuhitimisha Mkutano wa 47 wa Kamati Tendaji ya Kitaifa (National Oversight Committee -NOC), jijini Dodoma.

 

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban, ameongoza Mkutano wa 47 wa Kamati Tendaji ya Kitaifa (National Oversight Committee -NOC) inayosimamia utekelezaji wa miradi ya kuwezesha na kuboresha mazingira ya biashara nchini kwa ufadhili wa TradeMark Africa (TMA), kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Natu El- maamry Mwamba.

Mkutano huo umeidhinisha bajeti ya mwaka 2024/2025 kiasi cha dola za Marekani milion 7.1 ambayo itatekeleza miradi mbalimbali inayolenga kuongeza ufanisi wa biashara nchini na ukanda kwa ujumla ikiwa ni pamoja na kujenga uwezo kwa vijana na wanawake katika kufanya biashara hususan katika Eneo Huru la Biashara Barani Afrika (AfCFTA).

Mkutano huo pia umepokea na kujadili taarifa ya utekelezaji wa miradi ya TMA kwa mwaka 2023/2024 ambapo ilibainishwa kuwa kwa kipindi cha Julai 2023 - Juni 2024, miongoni mwa mafanikio ni kukamilika kwa Sera ya Biashara (National trade policy) ambayo itazinduliwa tareh 11 Julai 2024.

Mafanikio mengine ni kukamilika na kuzinduliwa kwa Mfumo wa Kieletronic wa Uwekezaji (Tanzania Investement Single Window System) ambao unawezesha wawekezaji kuomba vibali vya uwekezaji kwa njia ya mtandao.

MWISHO.