Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

TASAF KUNUFAIKA NA MSAADA WA SH. BIL 15 KUTOKA UINGEREZA

01 Jun, 2023
TASAF KUNUFAIKA NA MSAADA WA SH. BIL 15 KUTOKA UINGEREZA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Natu El- Maamry Mwamba na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Mhe. David Concar, wakipeana mikono baada ya kubadilishana Hati za makubaliano ya msaada wa takribani shilingi bilioni 15 kwa ajili ya Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini (TASAF), hafla iliyofanyika jijini Dodoma.

Tanzania imepokea msaada wa paundi milioni tano sawa na takribani shilingi bilioni 15 kutoka Serikali ya Ungereza kwa ajili ya awamu ya pili ya Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini (TASAF).

Makabidhiano ya Hati za makubaliano ya msaada huo yamefanyika jijini Dodoma kati ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Natu El- Maamry Mwamba na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Mhe. David Concar.

Akizungumza baada ya makabidhiano hayo, Dkt. Mwamba alisema kuwa utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini nchini Tanzania unaendelea vizuri jambo linalosababisha washirika wa maendeleo kuendelea kutoa misaada kwa ajili ya mpango huo.

Alisema kuwa amekutana na Balozi huyo wakiangazia masuala ya kunusuru kaya maskini lakini pia kuendelea kuimarisha ushirikiano wa kimaendeleo kati ya nchi hizo mbili ambao umedumu kwa muda mrefu.

Kwa upande wake Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Mhe. David Concar, alisema Uingereza ni rafiki mkubwa wa Tanzania katika nyanja mbalimbali za maendeleo, hivyo nchi yake itaendelea kufanya jitihada za kuhakikisha inatoa mchango wake katika kukabiliana na umasikini ili kuboresha hali ya maisha ya wananchi.

Mwisho.