Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2024/2025
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

TANZANIA YASISITIZA UMUHIMU WA TAKWIMU KIUCHUMI

28 Jul, 2024
TANZANIA YASISITIZA UMUHIMU WA TAKWIMU KIUCHUMI
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban, akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia Mhe. Innocent Shiyo, mara baada ya kufika katika Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania nchini Ethiopia, pamoja na ujumbe wa Tanzania baada ya kumalizika Kikao cha Kwanza cha Maandalizi ya Mkutano wa Nne wa Kimataifa wa Ugharamiaji kwa Maendeleo Endelevu (Fouth International Conference on Financing for Deveoplopment - FfD4, kilichofanyika mjini Addis Ababa nchini humo.
 
Serikali ya Tanzania imeushauri Umoja wa Mataifa kuanzisha mfumo thabiti wa takwimu utakaosaidia kupata taarifa sahihi kuhusu masuala ya uchumi kuelekea azimio la Ajenda ya Hatua ya Addis Ababa.
 
Wito huo umetolewa na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban, mjini Addis Ababa nchini Ethiopia, kwa niaba ya Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), wakati wa kufunga kikao cha kwanza cha Kamati ya Maandalizi ya Mkutano wa Nne wa Kimataifa wa Ugharamiaji kwa Maendeleo Endelevu (Fouth International Conference on Financing for Deveoplopment - FfD4 unaotarajiwa kufanyika mwakani.
 
Alisema kuwa mfumo huo wa takwimu utasaidia kupata taarifa sahihi na kwakuwa upatikanaji wa takwimu hizo ni muhimu hasa kwa nchi zinazoendelea kama Tanzania katika kusaidia ukuaji wa uchumi jumuishi.  
 
“Takwimu zitaongeza kwa kiasi kikubwa uwezo wetu wa kushughulikia changamoto za maendeleo kama vile umaskini, ukosefu wa usawa, mabadiliko ya hali ya hewa, masuala ya mazingira, amani, na haki” alisema Bi. Amina.
 
Katika hatua nyingine Bi. Amina ameushauri Umoja wa Mataifa kuwekeza katika mawazo ya ubunifu ili kusaidia nchi zinazoendelea katika kutumia teknolojia mpya za data, kutumia data iliyogawanywa kijinsia katika ufadhili wa maendeleo ili kutambua na kushughulikia usawa wa kijinsia.
 
Aliongeza kuwa ni vyema Umoja wa Mataifa itambue hitaji la njia kamili ambayo inaenea zaidi ya vipimo vya Pato la Taifa katika kutathmini maendeleo ya kitaifa na kutetea kupitishwa kwa viashiria vya pande nyingi.
 
Alisisitiza kuhusu Umoja wa Mataifa (UN) kutenga rasilimali  kwa ajili ya ukusanyaji wa data, usambazaji, na matumizi ili kuhakikisha kuwa kunakuwa na ufuatiliaji mzuri wa maendeleo kuelekea Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs).
 
MWISHO