Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2024/2025
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

TANZANIA NA EU KUIMARISHA USHIRIKIANO

11 Nov, 2024
TANZANIA NA EU KUIMARISHA USHIRIKIANO

Tanzania imeushukuru Umoja wa Ulaya (EU) kwa kuendelea kuwa miongoni mwa washirika wakubwa wa kimkakati wa maendeleo nchini kwa kuendelea kusaidia utekelezaji wa bajeti na sekta nyingine muhimu licha ya ukweli kwamba baadhi ya washirika wa maendeleo walijitoa.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt Natu El-maamry Mwamba, wakati akifungua kikao cha Majadiliano kwa ajili ya kusaidia bajeti ya Serikali ya Tanzania kupitia mradi wa Finance for Growth (Budget Support dialogue meeting for the Finance for Growth Programme). Kikao kilifanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam, ambapo kikao hicho kikijumuisha Wataalamu kutoka Serikali ya Tanzania na Umoja wa Ulaya.

Dkt. Mwamba alisema kuwa, Serikali inatambua mchango mkubwa wa Umoja wa ulaya katika kuchangia maendeleo ya nchi ambapo Kwa Mwaka wa Fedha uliopita - 2023/24 walisaidia kiasi cha Euro Milioni 40.819 sawa na fedha za Kitanzania Billioni 115.774 kwa ajili ya kuchangia utekelezaji wa miradi ya vipaumbele katika sekta ya Nishati, Uchumi wa Buluu, Digitali, usawa wa kijinsia na  uboreshaji wa majiji (Green and Smart Cities).

“Tumeshuhudia matokeo  makubwa chini ya Programu hii ya Finance for Growth  kuanzia kwenye maeneo ya kisera hadi mafanikio halisi ikiwemo kufuatilia maendeleo ya utekelezaji wa Awamu ya Nne ya Programu ya Marekebisho ya Usimamizi wa Fedha za Umma (Public Financial Management - Reform Programme IV), Mpango wa Corporate Plan-6 chini ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Mpango Mkuu wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha (Financial Sector Development Master Plan) katika mtazamo wa sera” alisema Dkt. Mwamba.

Dkt. Mwamba aliongeza kuwa, kwa  upande mwingine, msaada mkubwa umeelekezwa katika kukamilisha Mfumo wa Kitaifa wa Kutoa Hati Fungani za Kijani (Green Bonds), kuanzishwa kwa Mfuko wa Kitaifa wa Uwekezaji wa Mitaji (National Venture Capital Fund), kupungua kwa asilimia ya Kadirio la Kodi, kuongezeka kwa usajili wa walipa kodi na ongezeko la asilimia ya kiasi cha mikopo kwa Wajasiriamali Wadogo na wa Kati (MSME) kati ya jumla ya mikopo inayotolewa na benki na taasisi ndogo za fedha nchini.

Kwa Upande wake Mkuu wa Masuala ya Ushirikiano wa Umoja wa Ulaya hapa nchini (EU), Bw. Marc Stalmans, ameishukuru Tanzania kwa kuendelea kuwa mdau muhimu wa Umoja huo na msimamizi mzuri wa shughuli zake ambazo zina manufaa kwa wananchi wake.

“Tanzania ni mshirika wa karibu sana wa Umoja wa Ulaya katika mtazamo wa kiuchumi, na kwa hivyo, tunathamini sana ushirikiano tulionao na Tanzania na utakuwa na nguvu zaidi katika siku zijazo” alisema Bw. Stalmans

Bw. Stalmans aliongeza kuwa, Tanzania inafanya vyema kwa kutokuwa na kiwango kikubwa cha deni, ambacho ni kiwango cha deni kilicho chini ya asilimia 40%, ukifananisha na nchi nyingine za ukanda wa Afrika Mashariki, pia kuna fursa nyingi zinazoelekezwa kukuza sekta binafsi, jambo ambalo linaongeza chachu katika ukuaji wa Uchumi.

Kikao hicho kilihudhuriwa na Naibu Gavana wa Benki kuu ya Tanzania, Bi. Sauda Msemo, Kamishna Msaidizi wa Idara ya Fedha za Nje, Bw. James Msina, Kamishna Msaidizi wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, kutoka Wizara ya Fedha, Bi. Dionisia Mjema, Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali (IAG), Bw. Benjamin Magai, Mkuu wa Masuala ya Msaada kati ya Tanzania na Umoja wa Ulaya, Kitengo cha Uratibu na Ushirikiano, Bw. Jonathan Mpuya, pamoja na wataalamu wengine wa Serikali na Umoja wa Ulaya.