Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

TANZANIA KUWA MWENYEJI WA MKUTANO WA TATHIMINI WA BENKI YA DUNIA (IDA 20-MTR)

10 Oct, 2023
TANZANIA KUWA MWENYEJI WA MKUTANO WA TATHIMINI WA BENKI YA DUNIA (IDA 20-MTR)
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango-Zanzibar, Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum, ambaye anaongoza Ujumbe wa Tanzania katika Mikutano ya Mwaka ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), kwa niaba ya Waziri wa Fedha wa Tanzania ambaye pia ni Gavana wa Benki ya Dunia, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), akizungumza wakati wa mkutano na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayesimamia dirisha la IDA (International Development Association), Bw. Akihiko Nishio, kuhusu Mkutano wa Kimataifa wa Tathmini ya Muda wa Kati wa Mzunguko wa 20 wa Benki ya Dunia (IDA 20-Medium Term Review), ambapo Tanzania itakuwa mwenyeji wa mkutano huo utakaofanyika Zanzibar kuanzia tarehe 6 hadi 8 Desemba, 2023, ukizishirikisha zaidi ya nchi 100 duniani. Mazungumzo yao yamefanyika kando ya Mikutano ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) inayofanyika jijini Marrakech, nchini Morocco.
 
 
Tanzania itakuwa mwenyeji wa Mkutano wa Kimataifa wa Tathimini ya Muda wa Kati wa Mzunguko wa 20 wa Benki ya Dunia (IDA20 Medium Term Review) utakaofanyika Zanzibar kuanzia tarehe 6 hadi 8 Desemba, 2023, ukizishirikisha wajumbe zaidi ya 2590 kutoka matafaifa takribani 100 duniani.
 
Hayo yamebainishwa mjini Marrakech, nchini Morocco, wakati Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango, Mheshimiwa Dkt. Saada Mkuya Salum, alipokutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayesimamia dirisha la IDA (International Development Association), Bw. Akihiko Nishio, kando ya Mikutano ya mwaka ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) inayofanyika nchini humo.
 
Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum, anayeongoza Ujumbe wa Tanzania katika Mikutano hiyo kwa niaba ya Waziri wa Fedha wa Tanzania na Gavana wa Benki Dunia, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu, na Makamu huyo wa Rais wa Benki ya Dunia, Bw. Akihiko Nishio, wameeleza kuwa mkutano huo ni muhimu kwa maendeleo ya wanachama wake kwa kuwa utajadili fursa na changamoto zinazotokana na kukabiliana na umasikini.
 
Mhe. Dkt. Saada Mkuya amesema kuwa Tanzania ni mdau mkubwa wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa na kwamba mkutano huo utatoa fursa ya wajumbe watakaohudhiria mkutano huo kujionea maendeleo makubwa ya nchi yaliyopatikana kutokana na mikopo nafuu, misaada na ushauri wa kiufundi kutoka katika taasisi hizo kubwa za Fedha duniani.
 
Kwa upande wake, Makamu wa Rais wa Shirika la Fedha la Kimataifa anayesimamia dirisha la IDA linalojihusisha na utoaji wa mikopo nafuu na misaada kwa nchi zinazoendelea, Bw. Akihiko Nishio, alisema kuwa Tanzania imepiga hatua kubwa kimaendeleo na itakuwa fursa ya nchi nyingine kujifunza.
 
Alisema kuwa Benki ya Dunia inatumia takribani theluthi tatu ya fedha kwa ajili ya kuzisaidia nchi zinazoendelea zilizopo kusini mwa jangwa la Sahara kutekeleza miradi mbalimbali ya kimkakati ambayo lengo lake ni kukabiliana na umasikini. Amebainisha kuwa Tanzania imepata mafanikio makubwa ambayo yatakuwa kielelezo na ushawishi kwa nchi nyingine kuiga maendeleo haya.
 
Alisema kuwa Mkutano huu utakuwa wa kipekee kwa sababu kwa mara ya kwanza utahudhuriwa na Rais wa Benki ya Dunia, Bw. Ajay Banga, Viongozi waandamizi wa Benki ya Dunia, wawakilishi wa nchi zinazonufaika wa IDA, pamoja na wafadhili wanaochangia fedha katika dirisha la IDA.
 
Mwisho.