Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2024/2025
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

SWEDEN KUSAIDIA UJENZI WA SGR LOT 3&4

02 Feb, 2024
SWEDEN KUSAIDIA UJENZI WA SGR LOT 3&4
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Mhe. Charlotta Ozaki Macias, ambaye ameahidi kuwa nchi yake, kupitia Taasisi zake likiwemo Shirika la Dhamana la nchi hiyo (EKN), itashiriki kugharamia ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR kipande cha tatu kinachoanzia Makutupora mkoani Singida hadi Tabora na kipande cha nne kinachoanzia Tabora hadi Isaka.
 
Katika mazungumzo yao Mhe. Nchemba ameishukuru Sweden kwa kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya Tanzania, ikiwemo kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) Lot 2, kipande kinachoanzia Morogoro hadi Makutupora mkoani Singida, ambacho ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 96 na kwa utayari wa nchi hiyo kutoa fedha kwa ajili ya kujenga reli  kipande cha tatu na cha nne.
 
Wakizungumza katika mkutano huo, Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Mhe. Charlotta Ozaki Macias, aliyeambatana na Balozi wa Biashara Endelevu kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Sweden, Bi. Cecilia Ekholm, wamesifu uhusiano imara uliopo kati ya nchi hizo mbili na kuahidi kukuza zaidi uhusiano wa kiuchumi kwa faida ya pande hizo mbili.
 
Mhe. Balozi Macias alisema kuwa nchi yake inasubiri kukamilika kwa masuala yaliyokubaliwa ikiwemo masuala ya mazingira na jamii ambao utekelezaji wake unatarajia kukamilika hivi karibuni.
 
Ziara ya Balozi huyo wa Sweden Mhe. Charlotta Ozaki Macias, ni ufuatiliaji wa matokeo ya ziara ambayo Mhe. Dkt. Nchemba, aliongoza ujumbe wa Tanzania katika nchi za Scandinavia, ikiwemo Sweden, na kukutana na uongozi wa Shirika la Dhamana la nchi hiyo (EKN), ambalo limetoa usaidizi katika ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) upande wa malighafi ya ujenzi, vitendea kazi, mifumo ya umeme, mitambo na teknolojia.