Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2024/2025
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

STANDARD CHARTERED YAIPONGEZA TANZANIA KWA KUTHIBITISHWA NA MOODY’S DARAJA B1

24 Feb, 2026
STANDARD CHARTERED YAIPONGEZA TANZANIA KWA KUTHIBITISHWA NA MOODY’S DARAJA B1
Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) (kulia), akiagana na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered, Bw. Herman Kasekende aliyeambatana na ujumbe kutoka benki hiyo, baada ya kukutana na kufanya mazungumzo, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam, ambapo walijadili kuhusu masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Serikali na Benki hiyo.
 
Benki ya Standard Chartered, imeipongeza Tanzania baada ya Kampuni ya Kimataifa inayojihusisha na kufanya tathimini ya uwezo wa nchi kuyafikia masoko ya mitaji na dhamana ya kimataifa ya Moody's Investors Limited, kuithibisha kuwa katika kiwango cha daraja la B1 na Mtazamo thabiti.

Pongezi hizo zimetolewa jijini Dar es Salaam na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo, Bw. Herman Kasekende, alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), ambapo walijadiliana kuhusu masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Serikali na Benki hiyo, hususan ufadhili ya Reli ya Kisasa ya SGR.

Bw. Kasekende alisema kuwa Tanzania inafanya vizuri katika kusimamia uchumi wake ikiwemo kudhibiti mfumuko wa bei, kuimarisha thamani ya sarafu yake, kuongeza mauzo ya bidhaa nje ya nchi na usimamizi thabiti wa deni lake la Taifa, ikilinganishwa na nchi nyingi za Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Moody’s imeitathimini Tanzania kwa vigezo mbalimbali ambapo licha ya misukosuko kadhaa, umeiona nchi ikifanya maboresho yaliyofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika sekta mbalimbali za kiuchumi na kijamii.

Mwaka 2023, Kampuni hiyo, kwa mara ya kwanza, iliifanyia Tathimini Tanzania na kuipa Alama B2 na baadae mwaka 2024, baada ya Serikali kufanya mageuzi makubwa ya kiuchumi na kijamii ikaipatia Tanzania alama B1, inayoiwezesha kuyafikia Masoko ya Mitaji na dhamana kwa gharama nafuu pamoja na Kujenga Imani ya kuvutia mitaji ya uwekezaji kutoka nje ya nchi.

 
Mwisho