Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2024/2025
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

SHERIA MPYA YA UBIA MBIONI KUKAMILIKA

27 Apr, 2023
SHERIA MPYA YA UBIA MBIONI KUKAMILIKA

Kamishna wa idara ya ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP), Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. David Kafulila, akizungumza wakati akitoa mada kwenye semina elekezi kwa baadhi ya wahariri wa vyombo vya habari nchini, iliyolenga kuwajengea uelewa kuhusu utekelezaji wa sheria ya PPP, kwenye ukumbi wa Hazina Ndogo, jijini Arusha.

 

SERIKALI ipo katika hatua za mwisho za marekebisho ya Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP) ambapo hatua hizo zitawezesha utekelezaji wa miradi kuwa mzuri zaidi ikilinganishwa na huko nyuma.

Hayo yamesemwa na Kamishna wa Idara ya PPP Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. David Kafulila, wakati akiwasilisha mada kuhusu Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP) kwenye semina elekezi kwa baadhi ya wahariri wa vyombo vya habari nchini, iliyolenga kuwajengea uelewa wa masuala mbalimbali yanayotekelezwa na Wizara, iliyofanyika ukumbi wa Hazina ndogo, jijini Arusha.

Kamishna Kafulila alisema baada ya kukamilika kwa marekebisho ya Sheria, Tanzania itakuwa na sheria nzuri ya utekelezaji wa miradi ya PPP,  ambapo sheria hiyo inakuja pia kumlinda mwekezaji.

“Utekelezaji wa miradi ya PPP ulianza wakati wa Serikali ya Awamu ya Nne, ambapo mwaka 2009 ilitungwa sera ya PPP na mwaka 2010 ilitungwa sheria na kufuatiwa na kanuni zilizotungwa mwaka 2011, Sheria hii ilifanyiwa marekebisho mwaka 2014 na kufuatia marekebisho mengine ya sheria hiyo yaliofanyika mwaka 2018” alisema Kafulila.

Aliongeza kuwa, Kwa sasa marekebisho makubwa ya sheria hiyo yapo kwenye hatua nzuri na sheria inakuja kumlinda mwekezaji, tofauti na huko nyuma ambapo hakukuwa na sheria nzuri kwa ajili ya kuweza kutekeleza miradi kwa njia ya ubia.

“Wakati wa utekelezaji wa miradi ya PPP, miradi mingine itaibuliwa na kuletwa na sekta binafsi na mingine italetwa na Serikali na msingi wa PPP ni kuifanya sekta binafsi ifanye majukumu ambayo yangefanywa na Serikali” alisema Kafulila.

Semina hiyo ya siku mbili  ni moja ya njia za kimkakati katika utekelezaji wa Mkakati wa Mawasiliano wa Wizara (Communication Strategy) ambapo Wizara inakutana na wadau mbalimbali wakiwemo waandishi wa habari ili kuuhabarisha umma kuhusu shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na Serikali kupitia wizara hiyo.

MWISHO