Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2024/2025
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

SERIKALI YAWALIPA WAZABUNI TRIL 2.1 KWA MWAKA 2016 HADI 2023

30 Jan, 2024
SERIKALI YAWALIPA WAZABUNI TRIL 2.1 KWA MWAKA 2016 HADI 2023

Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akijibu swali la Mbunge wa Kisesa, Mhe. Luhaga Mpina, kuhusu kiasi cha fedha ambacho Serikali imewalipa wazabuni na wakandarasi wa ndani baada ya kuwasilisha madai yao na kufanyiwa uhakiki, bungeni Jijini Dodoma.

 

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), ameliambia Bunge, Mjini Dodoma kuwa katika kipindi cha Mwaka wa Fedha 2016/2017 hadi Desemba 2023, imewalipa wazabuni na wakandarasi wa ndani zaidi ya shilingi trilioni 2.1 kati ya madai ya zaidi ya shilingi trilioni 3.1 yaliyowasilishwa.

Dkt. Nchemba amesema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Kisesa, Mhe. Luhaga Mpina, aliyetaka kufahamu kiasi cha fedha ambacho Serikali imewalipa ama kukataa kuwalipa wazabuni na wakandarasi wa ndani baada ya kuwasilisha madai yao na kufanyiwa uhakiki.

“Jumla ya madeni ya wazabuni na wakandarasi yaliyowasilishwa kwa uhakiki yalikuwa zaidi ya sh. bilioni 3,110.33, kati ya kiasi hicho madeni yaliyolipwa ni zaidi ya sh. bilioni 2,128.54 ambapo sh. bilioni 1,032.13 ni madeni ya wazabuni na sh. bilioni 1,096.41 ni madeni ya wakandarasi” alisema Dkt. Nchemba

Alisema kuwa madeni ya sh. bilioni 981.79 yalikataliwa kutokana na sababu mbalimbali, ikiwemo kukosekana kwa nyaraka, madeni kubainika kulipwa tayari, pamoja na makosa ya ukokotoaji. 

Mhe. Dkt. Nchemba aliongeza kuwa Serikali kwa kutambua umuhimu na mchango wa Sekta Binafsi katika maendeleo na uchumi wa Taifa, imeendelea kutenga na kulipa madeni ya wazabuni na wakandarasi yaliyohakikiwa na kukubaliwa.

Alifafanua kuwa Serikali imeongeza bajeti ya kulipa madeni kutoka wastani wa shilingi bilioni 400 hadi shilingi bilioni 700 kwa mwaka na kuahidi kuwa madai ya wazabuni na wakandarasi yataendelea kulipwa kadri watakavyowasilisha hati zao za kukamilisha kazi (certificates).

Mwisho