Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2024/2025
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

SERIKALI YAHIMIZA MATUMIZI YA MASHINE YA KIELEKTRONIKI

28 Nov, 2024
SERIKALI YAHIMIZA MATUMIZI YA MASHINE YA KIELEKTRONIKI

Mwenyekiti wa Kongamano la Kodi, Bw. Robert Manyama, akitoa ufafanuzi wakati wa Kongamano la Kodi kwa wadau mbalimbali (hawamo pichani) lililofanyika katika Kanda ya Ziwa (Kigoma)

 

Serikali ina jukumu kubwa la kuweka mikakati ya kuendelea kurasimisha biashara nchini na kuhamasisha utumiaji wa mashine za kielektroniki katika utoaji wa risiti ikiwa ni pamoja na kutumia risiti hizo kujipatia zawadi kupitia Tuzo ya Uzalendo inayotarajiwa kufunguliwa rasmi hivi punde.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Kongamano la Kodi, Bw. Robert Manyama, wakati wa Kongamano la Kodi lililofanyika Mkoani Kigoma.

Bw. Manyama alisema, maoni mbalimbali yanayotolewa katika Makongamano hayo ya Kodi yatasaidia kuibua vyanzo vipya vya mapato na kupunguza utegemezi wa mikopo kutoka nje pamoja na kuendelea kubainisha maeneo yenye changamoto zaidi ili ziweze kupatiwa ufumbuzi.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo - TCCIA Mkoa wa Kigoma, Bw. Obadi Kabuga, alisema kuwa Kongamano hilo la Kodi limekuwa funzo na litasaidia Serikali kufanya biashara kwa kushirikiana na nchi zinazoizunguka, kwani sera zilizopo zinakinzana na sera za nchi jirani na kuiomba Serikali kufanya utafiti wa sera zake kabla ya kupeleka maboresho ya sera katika Bunge lijalo 2025/2026.

“Tunaomba mabadiliko ya Sera yatakapopelekwa Bungeni yafanyiwe utafiti kabla ya kufanya mabadiliko, wenzetu wana sera gani, ili zitakapokuja zile sera jumuishi ambazo zitakuwa na mfanano zitaleta uchumi mzuri na hususan katika Mkoa wetu wa Kigoma pamoja na Tanzania nzima” Alifafanua Bw. Kabuga.

Bw. Kabuga alihitimisha kwa kuishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuiamini TCCIA pamoja na Wizara ya Fedha kwa pamoja kuandaa Makongamano hayo ya Kodi Kikanda, ambapo mwitikio kwa wanakigoma ulikuwa mkubwa na wameitumia fursa hiyo vizuri kwa kutoa maoni na changamoto mbalimbali.

Kongamano hili la Kodi bado liko kwenye Kanda ya Ziwa (Kigoma),Makongamano haya ya Kikanda yalianzia Kanda ya Kati Dodoma, Kanda ya Kaskazini Arusha na yanaendelea katika Kanda nyingine.

 Mwisho