Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2024/2025
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

SERIKALI YAELEZA DHAMIRA YAKE KUWAWEZESHA VIJANA KIUCHUMI.

19 Apr, 2026
SERIKALI YAELEZA DHAMIRA YAKE KUWAWEZESHA VIJANA KIUCHUMI.

Naibu Waziri wa Fedha, Mhe, Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb), akizungumza katika Mahafali ya 20 ya Kidato cha Sita ya Shule ya Sekondari Thaqaafa, wilayani Nyamagana jijini Mwanza alipokuwa mgeni Rasmi katika mahafali hayo.

 

Serikali imeeleza dhamira yake ya kuendelea kuwawezesha vijana kiuchumi kupitia sera na mipango mbalimbali ya kiuchumi na kijamii.

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb), katika Mahafali ya 20 ya Shule ya Sekondari ya Thaqaafa, wilayani Nyamagana mkoani Mwanza.

Alieleza kuwa, Serikari inaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa vijana kupitia Sera na mipango mbalimbali ya kiuchumi na kijamii ili kuhakikisha kuwa vijana wanapata fursa za kuendeleza vipaji vyao na kuchangia kikamilifu maendeleo ya taifa.

‘’Dunia ya sasa inahitaji vijana wanaoweza kutatua changamoto kwa ubunifu, hasa katika nyanja za uchumi, teknolojia na ujasiriamali ‘’ Alisema Mhe. Munde (Mb).

Amewaasa vijana kuendelea kuwa na nidhamu na uadilifu kwakuwa Taifa linahitaji vijana wenye misingi imara ya maadili, wanaoweza kusimamia rasilimali za nchi kwa uwajibikaji na weledi.

Kwa upande wake Meneja wa Shule ya Thaqaafa, Bw. Idrisa Hayeshi, amewasisitiza wazazi kuendelea kushirikiana na walimu na Uongozi wa shule kufuatilia maendeleo ya wanafunzi ili kujua mwenendo wa tabia ambazo zina athari katika masomo yao.

“Shule imejipanga kutoa elimu bora ikiwa na matokeo mazuri kwa kila mwaka, tunavyofanya mawasiliano na mzazi ni kwamba atoe ushirikiano ili mtoto apate kitu kinachostahili’’ alisema Bw. Hayeshi.

Shule ya Sekondari  Thaqaafa imeadhimisha Mahafali ya 20 ya Kidato cha Sita ambayo yalihudhuriwa na wahitimu (50).

Mwisho