Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2024/2025
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

SERIKALI: TUMIENI MIKOPO KUWEKEZA KWENYE BIASHARA ZINAZOZALISHA

14 Mar, 2025
SERIKALI: TUMIENI MIKOPO KUWEKEZA KWENYE BIASHARA ZINAZOZALISHA
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Musoma mkoan Mara, Bw. Msongela Palela, akisoma kipeperushi alichokabidhiwa na Afisa Usimamizi wa Sekta ya Fedha Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha Wizaya ya Fedha Bw. Santley Kibakaya, chenye mada kuhusu uwekezaji ikiwa ni moja ya mada ambayo itafunzishwa wakati wa utoaji elimu ya fedha kwa wananchi wa Wilaya hiyo.
 
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Musoma, mkoani Mara, Bw. Msongela Palela, amewataka wananchi wa Wilaya hiyo kutumia mikopo wanayokopa kufanya uwekezaji unaozalisha faida  ili kuepuka kushindwa kufanya marejesho ya mkopo.
 
Bw. Palela alitoa rai hiyo wakati alipokutana na Timu ya Wataalamu kutoka Wizara ya Fedha, Taasisi za Serikali na Binafsi ambayo ipo mkoani Mara kutoa elimu ya fedha  kwa makundi mbalimbali.
 
"Kwenye Wilaya yetu kumekuwa na changamoto kwa wananchi wetu kuchukua mikopo na hawaendi kuwekeza kwenye maeneo ambayo yatazalisha faida ili watumie faida ile kufanya marejesho”, alisema Bw. Palela.
 
Aliongeza kuwa wananchi kukopa sio jambo baya lakini alitarajia mikopo hiyo iwasaidie lakini imekua tofauti kwa sababu haiendi kutumiwa katika shughuli za uzalishaji hivyo wanashindwa kufanya marejesho.
 
Bw. Palale alifafanua kuwa elimu ya fedha ni muhimu hivyo ni vyema Wizara ya Fedha ikahakikisha inawafikia wananchi wote na elimu hiyo iwe endelevu kwakuwa ina mchango mkubwa katika kuchangia uchumi wa nchi endapo itaeleweka kwa wananchi wote.
 
Aidha, alizitaka Taasisi za Fedha zinazojihusisha na utoaji mikopo, kufuata utaratibu na Sheria zilizowekwa na Serikali ili mikopo wanayotoa kwa wananchi iwasaidie na isiwe chanzo cha kuongeza tatizo  kwa kuweka riba kubwa zisizolipika kwa urahisi.
 
"Naendelea kuwaomba watoa huduma za fedha kuwa waaminifu na kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu zilizowekwa na Benki Kuu ya Tanzania za kuwalinda watoa huduma na wateja.
 
Vilevile, aliwataka Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Musoma kujenga utaratibu wa kutumia Taasisi rasmi zinazotambuliwa na Serikali wanapohitaji mikopo, ili kuepuka udhalilishaji unaofanywa na Taasisi ambazo haziko rasmi na hazifuati utaratibu.
 
Bw. Palela aliipongeza Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwa kuendelea kuwachukulia hatua watoa huduma wanaofanya biashara kinyume na utaratibu unavyoelekeza.
 
Naye mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo Bw. Mbagira Kajanja, aliishukuru Serikali kwa kuwapatia elimu ya fedha ambapo alieleza kupitia elimu hiyo imewafumbua macho na kuelewa baadhi ya taratibu ikiwemo kuwa na haki ya kusoma mkataba kabla ya kuchukua mkopo na kuelewa masharti ya mkopo na kujua viwango vya riba.
 
“Naamini baada ya elimu hii, tutabadilika na kutumia Taasisi rasmi zinazotambulika na Serikal, tutasoma mkataba kwa makini na kama hatujaelewa tutaomba tuelimishwe kabla ya kusaini”, alisema Bw. Kajanja.
 
Kwa upande wake Afisa Usimamizi wa Sekta ya Fedha Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha, Wizaya ya Fedha Bw. Santley Kibakaya, alisema kuwa Wizara inaendelea na zoezi la utoaji elimu ya fedha kwa wananchi ikiwa ni utekelezaji wa Mpango Mkuu wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha kwa mwaka 2021/2022 hadi 2029/2930.
 
Alisema kuwa hadi sasa Wizara ya Fedha imetoa elimu ya fedha katika mikoa 15, ikiwemo mkoa wa Kagera, Singida, Manyara, Kilimanjaro, Arusha, Kigoma, Pwani, Morogoro, Rukwa, Lindi, Mtwara, Tabora, Shinyanga, Simiyu na Mara.
 
Lengo la Wizara ni kwamba hadi kufikia mwaka 2025/2026 mikoa yote 26 ya Tanzania iwe imepata elimu ya fedha.
 
MWISHO.