Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2024/2025
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

SERIKALI KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIA NCHI

10 Dec, 2024
SERIKALI KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIA NCHI
Kamishna Msaidizi Idara ya Sera anayeshughulikia masuala ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Masuala ya Kodi na Mwenyekiti wa Kongamano la Kodi, Bw. Juma Mkabakuli, akifungua Kongamano la Kodi Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, kwa niaba ya Uongozi wa Wizara ya Fedha lililofanyika Mkoa wa Iringa.

 

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaendelea kupambana na uharibifu wa mabadiliko ya mazingira na tabia nchi, kuboresha usimamizi wa kodi, kuimarisha sekta ya fedha na sera za uchumi, kuendelea kulinda amani, usalama na utulivu wa ndani ya nchi, kuwekeza katika teknolojia kwa kupunguza gharama za uzalishaji, kuhakikisha upatikanaji na usalama wa chakula pamoja na kuibua vyanzo vipya vya mapato.
 
Hayo yameelezwa na Kamishna Msaidizi Idara ya Sera anayeshughulikia masuala ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Masuala ya Kodi na Mwenyekiti wa Kongamano la Kodi, Bw. Juma Mkabakuli, wakati akifungua Kongamano la Kodi kwa niaba ya Uongozi wa Wizara ya Fedha lililofanyika  Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Mkoani  Iringa.
 
“Sote tunatambua kwamba Dunia inaendelea kupambana na uharibifu wa mabadiliko ya tabia nchi, kuweka msisitizo kwa nchi zinazoendelea kuhakikisha tunakusanya mapato ya ndani ya kutosha hususani kwenye rasilimali asilia zilizopo na kuyatumia katika kufikia malengo ya maendeleo endelevu, (2030)  yaani sustainable development goals 2030, kuimarisha sekta ya fedha na sera za uchumi, kuendelea kulinda amani, usalama na utulivu wa ndani ya nchi, kuwekeza katika teknolojia kwa kupunguza gharama za uzalishaji, kuhakikisha upatikanaji na usalama wa chakula pamoja na kuweka mikakati ya kukabiliana na uhaba wa fedha za kigeni ili kuendelea kukuza sekta ya biashara na uwekezaji.”Alifafanua Bw. Mkabakuli.
 
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chemba ya Biashara,Viwanda na Kilimo – TCCIA Kanda ya Nyanda za 
Juu Kusini, Mkoa wa Iringa, Bw. Hamid Mbatta aliwaasa washiriki wa Kongamano la Kodi mkoa wa Iringa na Tanzania kwa ujumla kuendelea kulipa kodi kwa wakati kwa maendeleo ya nchi.
 
“Naishukuru Serikali kwa namna ambavyo sasa pesa ya kodi inavyotumika; sisi sote ni mashahidi msema kweli ni mpenzi wa Mungu, kazi zinazofanywa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hasa baada ya uchaguzi wa 2020 zimeonekana kwa macho, tukishuhudia reli ikijengwa, Barabara zikitengenezwa tena nzuri za kisasa, vituo vya afya vinajengwa, hospitali, vifaa tiba vinanunuliwa, shule zinafanyiwa ukarabati na mengine yanajengwa kwa kweli tunaona fedha zinavyotitirika na kuleta maendeleo. “Alifafanua Bw. Mbatta.
 
Naye Diwani wa Manispaa ya Iringa, Mhe. Devotha Chaula, alisema kuwa amefarijika sana kuwa mmojawapo walioshiriki katika Kongamano la Kodi Kikanda kwani amepata elimu ambayo atawafikishia Madiwani wenzake katika mikutano yao pamoja na wafanyabiashara. Lengo ni kuona kila Mtanzania ambaye anastahili kulipa kodi analipa kwa hiari.
 
“Niwashukuru sana TCCIA kwa kuja kutuelimisha, kuhusiana na suala la kodi, wamekuwa wakituelimisha Kiwilaya, Kimkoa lakini leo ni Kitaifa nimeona faida ya hili Kongamano, ambalo ni zuri lakini natamani hata safari hii tutakapoingia kwenye Baraza letu la Madiwani Iringa Manispaa niweze kulizungumzia hilo ili ujumbe kwa madiwani wenzangu ufike ili na wenzangu waweze kuongea kwenye Kata zao, kwa kufanya hivyo suala la kodi litawafikia kwa kina zaidi”. Alisema Mhe. Chaula.
 
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Masoko ya Manispaa ya Iringa, Bw. Raphael Ngullo, aliipongeza Serikali kwa kufuta na kupunguza baadhi ya ada na tozo kero takriban 379 hiyo inaonesha kuwa Serikali inafanyia kazi maoni mbalimbali yanayotolewa katika Makongamano haya.
 
“Kongamano hili limechukua maoni yetu, yale ambayo yanaleta usumbufu kidogo katika kodi wameyachukua. Lakini pia tunafurahi sana, tunashukuru sana kuambiwa Serikali imekwisha shughulikia kero mbalimbali za kodi, kodi 379 hilo ningependa niipongeze sana Serikali, kwamba ikituma watu kama ilivyowatuma leo inachukua maoni na inayafanyia kazi na inaleta mrejesho. Alifafanua Bw. Ngullo.
 
Kongamano hili la Kodi bado liko kwenye Kanda ya Nyanda za Juu Kusini (Iringa), yalianzia Kanda ya Kati Dodoma, na Kanda ya Kaskazini Arusha, Kanda ya Ziwa Mwanza na Kigoma na Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Mbeya na Iringa na yanaendelea katika Kanda nyingine. Kanda hii ya Nyanda za Juu Kusini Mkoa wa Iringa imeshirikisha wadau mbalimbali wakiwemo Madiwani, Wanasheria, Sekta ya Chai, Maziwa, Viwanda vya Mbao, Usindikaji, Wafanyabiashara wa Masoko, Hoteli, Pembejeo za Kilimo, Wadau wa Elimu, Wakulima, Washauri wa Kodi pamoja na Wasafirishaji wa Bajaji.
 
Mwisho