Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2024/2025
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

SERIKALI KUHAKIKISHA MISAMAHA YA KODI INATUMIKA IPASAVYO

25 Apr, 2023
SERIKALI KUHAKIKISHA MISAMAHA YA KODI INATUMIKA IPASAVYO

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb) alipokuwa akijibu swali, bungeni jijini Dodoma.

 

Serikali imesema inaendelea kutekeleza sheria katika ufuatiliaji na tathmini ya misamaha ya kodi ikiwemo Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ili kuhakikisha kuwa misamaha ya kodi inatolewa kwa kuzingatia sheria na inatumika kama ilivyokusudiwa.

Hayo yameelezwa bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb) alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Kibamba, Mhe. Issa Jumanne Mtemvu aliyetaka kujua mkakati wa Serikali kuhakikisha Misamaha ya VAT inayotolewa inaleta tija kama ilivyokusudiwa.

Mhe. Chande alisema ili kuhakikisha misamaha ya kodi inakuwa na tija katika uchumi na jamii kwa ujumla, orodha ya bidhaa na vifaa vinavyostahili msamaha wa kodi inaandaliwa na kuhakiki orodha ya bidhaa na vifaa.

“Tunahakikisha mwombaji anajaza fomu maalum inayothibitisha ununuzi wa bidhaa au vifaa husika pamoja na kufanya kaguzi za mara kwa mara dhidi ya misamaha iliyotolewa ili kuthibitisha iwapo matumizi ya bidhaa au vifaa vilivyosamehewa kodi vimetumika kama ilivyokusudiwa”, aliongeza Mhe. Chande.

Alisema pia Wizara ya Fedha na Mipango kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania inaendelea kutekeleza matakwa ya kisheria katika ufuatiliaji na tathmini ya misamaha ya kodi ikiwemo Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ili kuhakikisha kuwa misamaha ya kodi inatolewa kwa kuzingatia sheria na inatumika kama ilivyokusudiwa.

Mwisho.