Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2024/2025
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

SERIKALI KUENDELEA KUBORESHA UANDAAJI WA MIPANGO NA BAJETI.

21 Aug, 2026
SERIKALI KUENDELEA KUBORESHA UANDAAJI WA MIPANGO NA BAJETI.

Mhasibu Mkuu Msaidizi wa Serikali, Wizara ya Fedha, Bw. Ayubu Banzi, akifungua kikao kazi cha Tathmini ya Uandaaji na Utekelezaji wa Bajeti kwa wataalamu wa Mipango na Bajeti kundi la pili kati ya makundi matatu yanayoshiriki mafunzo ya Tathmini ya Uandaaji na Utekelezaji wa Bajeti kwa watalaam kutoka wizara, idara zinazojitegemea, wakala za Serikali na sekretarieti za mikoa na mamlaka ya Serikali za mitaa, kinachofanyika Treasury Square Dodoma.   

 

Serikali imeeleza kuwa inaendelea kuboresha uandaaji wa mipango na bajeti ili kuongeza ufanisi katika utekelezaji na usimamizi wa bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2027/28–2029/30.

Hayo yameelezwa katika Ukumbi wa Kambarage, Treasury Square, jijini Dodoma na Mhasibu Mkuu Msaidizi wa Serikali, Wizara ya Fedha, Bw. Ayubu Banzi, kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Natu El-Maamry Mwamba, wakati akifungua kikao kazi cha Tathmini ya Uandaaji na Utekelezaji wa Bajeti kwa wataalamu wa Mipango na Bajeti kundi la pili kati ya makundi matatu yanayoshiriki mafunzo hayo.

Bw. Banzi alisema kikao hicho ni muhimu kwa kuwa kitatoa fursa kwa washiriki kutoa maoni yatakayotumika kuboresha na kuongeza ufanisi katika utekelezaji na usimamizi wa bajeti ya Serikali. 

Alisema maoni hayo pia yatasaidia kuboresha Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2027/28–2029/30.

Kikao hicho kimewahusisha wataalamu wa masuala ya mipango na bajeti kutoka wizara, idara zinazojitegemea, wakala za Serikali, Sekretarieti za Mikoa pamoja na Mamlaka za Serikali za Mitaa. 

Lengo la kikao hicho ni kuhakikisha kuwa wataalamu wanaendelea kuwa na uelewa na uwezo unaohitajika katika maandalizi, utekelezaji na usimamizi wa mipango na bajeti ya Serikali.

Mwisho.