Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2024/2025
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

NSUBILI JOSHUA AWATAKA WATENDAJI WA WIZARA YA FEDHA KUENDELEA KUCHAPA KAZI

13 Feb, 2026
NSUBILI JOSHUA AWATAKA WATENDAJI WA WIZARA YA FEDHA KUENDELEA KUCHAPA KAZI

Naibu Katibu Mkuu Huduma za Hazina Wizara ya Fedha, Bw. Nsubili Joshua, akitoa rai kwa Wakuu wa Idara na Vitengo Fungu 50 Wizara ya Fedha kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kwa wakati ili kuwa na matokeo Chanya katika kuhakikisha Wizara inatoa mchango mkubwa katika maendeleo ya nchi, kilichofanyika Ofisi za Wizara ya Fedha, Treasury Square, Wizara ya Fedha, jijini Dodoma.

 

Naibu Katibu Mkuu (Huduma za Hazina) Wizara ya Fedha, Bw. Nsubili Joshua, amewataka Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara hiyo kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa bidii, weledi na kwa kuzingatia muda, ili kuhakikisha Wizara inatoa mchango mkubwa na wenye tija katika maendeleo ya Taifa.

Bw. Joshua ametoa wito huo wakati wa kikao kazi na Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara (Fungu 50) kilichofanyika Ofisi za Wizara ya Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma.

Amesisitiza umuhimu wa uwajibikaji, ushirikiano na ubunifu katika utekelezaji wa majukumu ya kila siku, ili kuongeza ufanisi na kufikia malengo yaliyowekwa.

Kwa upande wao, Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara ya Fedha (Fungu 50) wameahidi kuendelea kufanya kazi kwa bidii, uadilifu na mshikamano, pamoja na kuahidi kumpa ushirikiano wa kutosha kiongozi huyo, ili kuhakikisha utekelezaji mzuri wa majukumu ya Wizara, ikiwemo usimamizi wa sera za uchumi na programu mbalimbali za maendeleo.

Mwisho