Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2024/2025
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

NAIBU KATIBU MKUU, ELIJAH MWANDUMBYA ATEMBELEA BANDA LA WIZARA YA FEDHA SABASABA

12 Jul, 2024
NAIBU KATIBU MKUU, ELIJAH MWANDUMBYA ATEMBELEA BANDA LA WIZARA YA FEDHA SABASABA

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya (katikati), akitembelea Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere Barabara ya Kilwa, Temeke, jijini Dar es Salaam, ambapo amepongeza mikakati iliyowekwa ya kutoa elimu kwa umma kuhusu majukumu ya Wizara na Taasisi zake. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha, Bw. Benny Mwaipaja na Kushoto ni Afisa Mwandamizi wa Kitengo hicho, Bw. Ramadhani Kissimba.  

 

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya ametembelea Banda la Wizara ya Fedha katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere Barabara ya Kilwa, Temeke, jijini Dar es Salaam, ambapo amepongeza mikakati iliyowekwa ya kutoa elimu kwa umma kuhusu majukumu ya Wizara na Taasisi zake.

Bw. Mwandumbya alisema kuwa Wizara ya Fedha ni Wizara muhimu katika kuchochea maendeleo ya mchi hivyo ni muhimu elimu ikatolewa kwa usahihi na ufanisi ili watanzania waweze kuelewa majukumu ya Wizara na Taasisi zake.

Amesema kuwa Maonesho hayo ambayo Idara, Vitengo na Taasisi za Wizara ya Fedha kwa pamoja zinatoa nafasi kwa watanzania kupata elimu kwa urahisi kuhusu Wizara hiyo.

Bw. Mwandumbya amewataka Wananchi kutembelea Banda la Wizara hiyo ili wapate elimu na huduma za kibenki, mifuko ya dhamana ya uwekezaji, Sera, masuala ya sekta ya fedha, usuluhishi wa masuala ya kodi, vyuo vya elimu ya juu, ununuzi na ugavi, pemsheni na mirathi,

Mwisho.