Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2024/2025
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

MIVUTANO BAINA YA WATUMISHI NA WAKOPESHAJI WASIO RASIMI HUATHIRI UTENDAJI KATIKA SEHEMU ZA KAZI

07 Jun, 2024
MIVUTANO BAINA YA WATUMISHI NA WAKOPESHAJI WASIO RASIMI HUATHIRI UTENDAJI KATIKA SEHEMU ZA KAZI
Afisa Usimamizi wa Fedha katika Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha katika Wizara ya Fedha, Bw. Stanley Kibakaya, akitoa semina kwa wananchi wa kata ya Kibondo mkoani Kigoma, kuhusu umuhimu wa elimu ya fedha na njia bora za kujikwamua kiuchumi na kibiashara.
 
Watumishi wa umma wilayani Kibondo mkoani Kigoma, wametakiwa kuacha tabia ya kujihuisha na ukopaji  wa fedha katika taasisi zisizo rasmi ambazo maranyingi huwa na riba kubwa na kusababisha migogoro wanaposhindwa kulipa kwa wakati.
 
Akizungumza na timu ya wataalamu wa fedha kutoka wizara ya fedha, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo, Dkt. Gabriel Chitupila,  alisema kuwa mivutano baina ya watumishi na wakopeshaji wasio rasmi huathiri utendaji katika sehemu za kazi na kuhatarisha utumishi wa mkopaji.
 
Dkt. Chitupila alisema kuwa hali hiyo husababisha kushusha ari ya watumishi kufanyakazi kutokana na muda mwingi wakijikuta wanakimbizana na wakopeshaji hasa pale mkopo unapokuwa mkubwa na kushindwa kulipa hivyo akawasihi kama kuna ulazima wa kukopa wazitumie taasisi ambazo zimesajiliwa ili wapate huduma yenye uhakika isiyo kandamizi.
 
“tatizo la mikopo “kausha damu” lipo na linawakumba hadi watumishi wa umma hasa walimu, unakuta mwalimu hakai ofisini akiogopa kutafutwa na wakopeshaji au kulazimika kutoroka katika kituo chake cha  kazi kwenda kufanya vibarua sehemu nyingine ili pate hela za kulipa deni na kusababisha wanafunzi kukosa haki yao ya msingi ya kufundishwa, nitoe rai wenye tabia hiyo waache mara moja” alıonya Dkt. Chitupila.
 
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kibondo,  Kanali Agrey Magwaza, aliwahimiza Maafisa Maendeleo ya Jamii na Waratibu wa Huduma Ndogo za Fedha ngazi ya Halmashauri kufuatilia na kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za kifedha  ili kuwasaidia kuwa na uelewa juu ya masuala mbalimbali ya huduma hizo.
 
" Maafisa Maendeleo ya Jamii na Waratibu wa Huduma za Kifedha katika halmashauri tufahamu kuwa kipimo chetu sisi watumishi wa umma ni namna tunavyo wahudumia wananchi na kuona wanavyoridhika na huduma kwa kulimaliza tatizo la kuwepo kwa watoa huduma wanaoweka riba kubwa na kukiuka sheria za nchi, hicho ndicho kitakuwa kipimo chetu cha utumishi". Alisema Kanali Magwaza.
 
Aidha, Magwaza alisema kuwa ni rahisi sana mtu kukopo wakati anaona riba ni kubwa lakini akianza kukatwa fedha ndio anaona fedha ni kubwa na mwishowe anajuta.
 
"Mtu anaona riba ni kubwa lakini anaona sawa tu na anapoanza kukatwa fedha zake ndipo anakunywa ba msongo wa mawazo na hatimaye mtu huyo anapoteza mwelekeo". Alisisitiza Kanali  Magwaza.
 
Mwisho