Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2024/2025
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

MHE. RAIS DKT. MWINYI AMEKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA WAZIRI WA FEDHA BALOZI OMAR.

19 Feb, 2026
MHE. RAIS DKT. MWINYI AMEKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA WAZIRI WA FEDHA BALOZI OMAR.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa  Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), mazungumzo yaliyofanyika Ikulu Zanzibar, leo tarehe 18 Februari, 2026.                                                                                                                                                                Waziri wa Fedha Mhe. Balozi Omar, aliambatana na Manaibu Waziri wake Mhe. Laurent Deogratius Luswetula (Mb) na Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb), pia   Naibu Katibu Mkuu, Bi. Amina Khamis Shaaban.

Waziri wa Fedha alifika Ikulu Zanzibar  kwa lengo la kujitambulisha baada ya kuteuliwa kuongoza Wizara ya Fedha na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hivi karibuni.