Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

MHE.MWIGULU AWATAKA MAMLAKA YA MAPATO TANZANIA (TRA) KUSAIDIA KUKUZA SEKTA BINAFSI NCHINI

03 Oct, 2023
MHE.MWIGULU AWATAKA MAMLAKA YA MAPATO TANZANIA (TRA) KUSAIDIA KUKUZA SEKTA BINAFSI NCHINI

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), akiwasili katika Ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) zilizopo katika mpaka wa Tanzania na Malawi wa Kasumulu Wilayani Kyela, mkoani Mbeya. Kushoto kwake ni Meneja Msaidizi wa Fordha kutoka Mamalaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Mbeya, Bw. Nsajigwa Mwambegele.

 

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), ameiagiza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kusaidia kukuza Sekta Binafsi nchini ambayo itasaidia kuongeza kipato, kukuza uchumi wa nchi na itatoa fursa kwa vijana wengi kujiajiri.

 
Mhe. Dkt. Nchemba alitoa maagizo hayo wakati akiongea na wananchi wa Kilambo, Kata ya Njisi Wilayani Kyela, Mkoani Mbeya, mara baada ya kufanya ziara yake ya kukagua shughuli za kiuchumi na maendeleo katika Kituo cha Forodha cha Pamoja-Kasumulu kilichopo mpakani mwa Tanzania na Malawi.
 
Alisema kuwa dhamira ya nchi ni kutaka kukuza Sekta Binafsi, hivyo ni lazima kuwe na nidhamu katika kuisimamia Sekta Binafsi hasa kwa kulinda mitaji ya vijana walioamua kujiajiri na kuajiri vijana wenzao na si kuua mitaji yao.
 
‘’Ni lazima tuwe na nidhamu katika sekta binafsi na tuache ubosi katika mitaji ya watu, na kama kijana ameamua kuanzisha shughuli yake na hajaisajili msimfungie biashara badala yake mleteeni hiyo leseni ambayo hana, msiharibu mtaji wake ili vijana wengi wajiajiri’’ alisema Mhe. Dkt. Nchemba
 
Aidha, Mhe.Dkt. Nchemba aliwataka wananchi kujenga tabia ya kulipa kodi na kuheshimu sheria za nchi ili kuongeza idadi ya walipa kodi, jambo ambalo litasaidia kushusha viwango vya ulipaji kodi na kuwapunguzia mzigo mkubwa wale wanaolipa kodi.
 
 Aliongeza kuwa matamanio ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa  Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ni kuona viwango vya kodi vinashuka ili kuchochea maendeleo ya kila Mtanzania.
 
‘’Natoa rai hapa wakati tunawasisitizia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kutekeleza maelekezo ya Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kukusanya mapato kwa weledi na kufuata kanuni, tunawasisitiza pia wananchi mjenge utaratibu wa kulipa kodi, kuheshimu sheria ili tunapokwenda! tukilipa wengi, tuweze kushusha viwango vya kodi’’ Aliongeza Mhe. Dkt. Nchemba
 
Awali akizungumza na Uongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Uongozi wa Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya, Mhe. Dkt. Nchemba aliwataka kuhakikisha wanadhibiti na kuwachukulia hatua kali za kisheria wale wote wanaofanya biashara za magendo katika mpaka wa Kasumulu, vitendo vinavyoikosesha Serikali mapato.
 
Katika ziara hiyo, Mhe. Dkt.  Nchemba aliongozana na Waziri wa Ujenzi, Mhe. Innocent Bashungwa (Mb), Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Juma Homera na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi Mkoani humo.
 
Mwisho