Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2024/2025
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

MHE. MUNDE AHIMIZA UTEKELEZAJI WA MRADI WA MADINI YA GRAPHITE MOROGORO

23 Apr, 2026
MHE. MUNDE AHIMIZA UTEKELEZAJI WA MRADI WA MADINI YA GRAPHITE MOROGORO

Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb) (wa nne kulia) na Kiongozi wa Ujumbe wa Kampuni ya Faru Graphite Corporation Limited  ambaye pia ni Afisa Mkuu wa Fedha wa Kampuni hiyo, Bw. Paul Sims, wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa pande hizo mbili, baada ya mkutano utekelezaji wa mradi wa uchimbaji wa madini ya Graphite Morogoro, uliofanyika Ofisini kwake, Treasury Square, jijini Dodoma.

 

Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb), amehimiza utekelezaji wa Mradi wa uchimbaji  madini ya Graphite uliopo  Mahenge Mkoa wa Morogoro ili uanze kutoa manufaa yaliyotarajiwa kwa watanzania kwa wakati.

Rai hiyo imetolewa Ofisini kwake jijini Dodoma wakati wa mkutano kati yake na Ujumbe wa Kampuni ya Faru Graphite Corporation Limited  ulioongozwa na Afisa Mkuu wa Fedha wa Kampuni hiyo, Bw. Paul Sims.

Mhandisi Munde alisema kuwa, Serikali itaendelea kutoa msaada katika kufanikisha utekelezaji wa mradi huo unaokwenda sambamba na wajibu wa mwekezaji katika masuala ya uwazi, utii wa masharti yaliyowekwa na ushirikiano wa karibu na mamlaka husika kadri utekelezaji unavyoendelea.

“Napenda kuihimiza kampuni yenu kuhakikisha kuwa mchakato wa upatikanaji wa mtaji unakamilika ndani ya muda uliokubaliwa ili kuanza utekelezaji wa mradi na kwamba fedha hizo zinaelekezwa kwa mujibu wa taratibu zilizokubaliwa”, alisema Mhandisi Munde

Alisema kuwa Serikali inatarajia mchango wa mradi huo katika upatikanaji wa ajira, kukuza fursa za biashara za ndani, kuongeza mapato ya fedha za kigeni, kuendeleza mnyororo wa thamani wa madini ya Graphite, kukuza viwanda, pamoja na kuongeza mapato ya muda mrefu ya Serikali yanayotokana na ushiriki wake katika mradi huo.

Vile vile alieleza kuwa mradi huo utatoa kipaumbele kwa maudhui ya ndani (local content), ikiwemo matumizi ya bidhaa na huduma za ndani, na pale ambapo ushiriki wa nje utahitajika, kutakuwa na utaratibu unaohakikisha ushiriki wa wazawa usiopungua asilimia 30, kwa kuzingatia makubaliano yaliyopo.

Aidha, Mhandisi Munde aliihakikishia Kampuni hiyo kuwa Serikali itaendelea kuunga mkono uwekezaji wa kimkakati unaoendana na vipaumbele vya maendeleo ya Taifa ikizingatiwa kuwa mradi huo ni sehemu ya nafasi ya kimkakati ya Tanzania katika madini muhimu duniani.

Kwa upande wake Kiongozi wa Ujumbe wa Kampuni ya Faru Graphite Corporation Limited  ambaye ni Afisa Mkuu wa Fedha wa Kampuni hiyo, Bw. Paul Sims, alisema kuwa mradi utasaidia katika maendeleo ya viwanda na kuimarisha nafasi ya Tanzania katika usambazaji wa madini muhimu yanayotumika katika uzalishaji wa kisasa na teknolojia za nishati safi.

Bw. Sims ameahidi kuongeza jitihada katika kuhakikisha mtaji unapatikana kwa haraka na kuanza kwa utekelezaji wa mradi huo na aliomba Serikali kuendeleza ushirikiano na wadau muhimu ili kufanikisha mradi huo kuanza kwa wakati.

Mwisho.