Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2024/2025
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

MHE. BALOZI OMAR AZUNGUMZA NA UONGOZI WA TWIGA CEMENT

20 Jan, 2026
MHE. BALOZI OMAR AZUNGUMZA NA UONGOZI WA TWIGA CEMENT

Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb)(Katikati), akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Kampuni ya Twiga Cement, Meneja Mkuu Kampuni ya Twiga Cement Bw. Alfonso Velez (kulia) na Mjumbe wa Bodi wa Kampuni hiyo, Bw. Raymond Mbilinyi, baada ya kikao chao kilichojadili masuala mbalimbali yanayohusu uendelezaji wa uwekezaji wa Kiwanda cha Saruji cha Twiga, kilichofanyika katika Ofisi za Wizara ya Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma.
 

Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na uongozi wa Twiga Cement ukiongozwa na Meneja Mkuu wake, Bw. Alfonso Velez, Ofisi za Wizara ya Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma,  ambapo pande hizo zimejadili masuala mbalimbali yanayohusu uendelezaji wa uwekezaji wa Kiwanda cha Saruji cha Twiga.

Mhe. Balozi Omar, aliuhakikishia uongozi huo kuwa Serikali itaendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini ili kuimarisha sekta ya viwanda.

Kwa upande wake Meneja Mkuu wa Kampuni hiyo Bw. Alfonso Velez, alisema kuwa lengo la kampuni ni kuendelea kukuza uwekezaji nchini ili kukidhi mahitaji ya soko pamoja na kutoa ajira kwa wananchi.

Kikao hicho kilihudhuriwa pia na Kaimu Kamishna wa Idara ya Uchambuzi wa Sera Dkt. Remidius Ruhinduka, Kamishna Msaidizi wa Idara ya Uchambuzi wa Sera, Bw. William Mhoja, Kamishna Msaidizi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mcha Hassan Mcha, Kamishna Msaidizi Idara ya Sheria -TRA, Bw. Gabriel Kimweri, Mjumbe wa Bodi wa Twiga cement, Bw. Raymond Mbilinyi na Mkurugenzi wa Fedha wa Twiga Cement, Bw. Simon Renauld, Meneja Biashara Mwandamizi wa Kampuni hiyo, Mhandisi Danford Semwenda na maafisa waandamizi Wizara ya Fedha.

MWISHO