Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2024/2025
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

MABEHEWA YA SGR KUKAMILIKA KWA WAKATI KOREA

26 Sep, 2023
MABEHEWA YA SGR KUKAMILIKA KWA WAKATI KOREA

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Bi. Amina Khamis Shaaban, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkuu wa Kituo cha Utafiti na Majaribio Dongjin Son, wakati alipokuwa akitoa ufafanuzi wa maendeleo ya utengenezaji wa mabehewa na vichwa vya treni ya mwendo kasi, ujumbe kutoka Tanzania ulipotembelea kiwanda hicho Changwon, Korea Kusini. Kushoto ni Kamishna Msaidizi Idara ya Fedha za Nje Bw. Melckzedeck Mbise.

 

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Bi. Amina Khamis Shaaban, ameeleza kuridhishwa na maendeleo ya utengenezaji wa mabehewa na vichwa vya treni, na Treni ya mwendokasi vinavyotengenezwa na kampuni za Hyundai Rotem na Sing Sung Rolling Stock Technology (SSRST) za Korea Kusini.

Alisema hayo mara baada ya kutembelea kampuni hizo zilizopo katika mji wa Changwon, Korea ya Kusini, zilizoingia mkataba na Serikali ya Tanzania, wa kutengeneza mabehewa 59 na vichwa vya treni 17 pamoja treni za Mwendokasi (Electric Multiple Unit) 10.

‘‘Kwa kampuni zote mbili maendeleo ni mazuri kwa hatua iliyofikiwa na wametueleza kuwa wanatarajia kukamilisha utengenezaji wa mabehewa na vichwa vya treni kama ilivyoainishwa katika makubaliano, na kwa kweli tuliyoyaona yako katika hali nzuri’’alisema Bi. Amina.

Aidha, alitumia nafasi hiyo kutoa maelekezo kwa sekta husika kuhakikisha kuwa inatoa mafunzo kwa watakao husika na kuendesha, kuhudumia treni hizo wanajengewa uwezo ili ziweze kudumu kwa muda mrefu na kutoa huduma bora kwa uendelevu.

‘‘Tunashauri wenzetu watakaosimamia uendeshaji wa treni hizi kwa Tanzania wajengewe uwezo wa uendeshaji na utunzaji ili mabehewa na vichwa viendelee kuwa na ubora huu kwa ajili ya huduma na pia yaweze kudumu kwa muda mrefu’’, alisisitiza Bi. Amina.

Ujumbe wa Tanzania ulikuwa Busan Korea ya Kusini kuhudhuria mkutano wa saba wa Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Korea Kusini na Nchi za Afrika (KOAFEC), Mjini Busan, Jamhuri ya Korea Kusini ambapo Tanzania iliungana na nchi nyingine za Afrika katika mkutano huo.

MWISHO.