Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

MAADHIMISHO WIKI YA HUDUMA ZA FEDHA KUWASOGEZEA WANANCHI HUDUMA ZA FEDHA KARIBU

21 Nov, 2022
MAADHIMISHO WIKI YA HUDUMA ZA FEDHA KUWASOGEZEA WANANCHI HUDUMA ZA FEDHA KARIBU

Serikali inafanya maadhimisho ya pili ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa ili wananchi waweze kupata elimu ya fedha na kuweza kufahamu fursa, bidhaa na huduma mbalimbali zilizopo kwa lengo la kujiongezea kipato na kukuza uchumi wa nchi.

Hayo yameelezwa jijini Mwanza na Kamishna wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Charles Mwamwaja alipokutana na wanahabari wakati akizungumza kuhusu maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa inayofanyika mkoani humo kuanzia Novemba 21 hadi 26, 2022.

Dkt. Mwamwaja alisema katika maadhimisho hayo elimu ya fedha kuhusu sera, sheria, huduma na bidhaa mbalimbali zilizopo katika Sekta ya Fedha zitatolewa pamoja na kuwakutanisha wanachi na wasimamizi wa huduma hizo.

“Maadhimisho haya ni muendelezo wa utekelezaji wa Mpango Mkuu wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha wa Mwaka 2020/21 – 2029/30 ambao pamoja na mambo mengine unalenga kutoa elimu ya fedha kwa umma kupitia maadhimisho haya “, alisema Dkt. Mwamwaja.  

Alisema kuwa pamoja na mambo mengine Serikali itapokea maoni mbalimbali ya kuboresha namna ya upatikanaji wa huduma za fedha ili kuhakikisha wananchi wote wanakuwa na uelelewa wa masuala hayo muhimu kwa uchumi wa nchi.

Aidha, aliwakaribisha wananchi wote hususan wa Mkoa wa Mwanza na mikoa ya jirani kushiriki katika maonesho hayo na kubainisha kuwa Serikali ipo tayari kuwapokea wananchi kwa wingi wao.

Naye, Kamishna Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Sekta ya Fedha, Bi. Dionisia Mjema alisema katika maadhimisho hayo kutakuwa na darasa maalum la kufundisha masuala mbalimbali yanayohusu Sekta ya Fedha ambayo yatakafundishwa na wataalam wa masuala ya fedha kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Benki Kuu ya Tanzania, Mamlaka ya Usimamizi wa Bima, Malaka ya Usimamizi wa Masoko ya Mitaji, Ofisi ya Waziri Mkuu Idara inayohisika na Usimamizi wa Hifadhi ya Jamii na Tume ya Maendleo ya Ushirika pamoja na Ofisi ya Rais TAMISEMI.

Alisema wananchi watafundishwa mada kuhusu Sera , Sheria na Kanuni za Sekta ya Fedha, usimamizi wa fedha binafsi, mikopo, bima, maisha baada ya kustaafu, uwekezaji pamoja na kutambua watoa huduma za fedha na wasimamizi wake.

Kwa upande wa washiriki wengine wa maadhimisho hayo walisema wako tayari kuwahudumia wananchi ili kuhakisha Serikali inatimiza lengo lake la kuhakisha takribani asilimia 80 ya wananchi wamepata uelewa wa masuala ya fedha ifikapo mwaka 2025.

 

Mwisho.