Category Title

 • Government Budget Speeches
 • Ministry's Budget Speeches
 • Budget Books 2024/2025
 • Budget Books 2023/2024
 • Budget Books 2022/2023
 • Budget Books 2021/2022
 • Budget Books 2020
 • Budget Books 2018/2019
 • Budget Books 2015/2016
 • Budget Books 2014/2015
 • Content not found
 • Content not found
 • Content not found

KATIBU MKUU -HAZINA AFANYA MAZUNGUMZO NA TIMU YA TMEA

16 Sep, 2022
KATIBU MKUU -HAZINA AFANYA MAZUNGUMZO NA TIMU YA TMEA

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Emmanuel Tutuba, amekutana na kufanya mazungumzo na timu ya Taasisi ya TradeMark East Afrika (TMEA) leo jijini Dar es Salaam ambapo kulikuwa na utambulisho wa Afisa Mtendaji Mkuu mpya wa TMEA Bw. David Beer ambaye alianza kazi rasmi tarehe 01 mwezi Septemba 2022, na aliambatana na Afisa Mtendaji Mkuu aliyemaliza muda wake Bw. Frank Matsaert.

Akizungumza katika majadiliano hayo Bw. Tutuba alisema Taasisi ya TMEA ni  wadau muhimu  ambao tumekuwa tukifanya nao kazi muda mrefu, na kusema kuwa Shirika hili lilianzishwa mwaka 2010 kwa dhumuni la kufanya shughuli zake Afrika ikiwemo kuongeza wigo wa biashara ambayo imewezesha mashirika ya maendeleo ya nchi mbalimbali zikiwemo Belgium, Canada, Dernmark, European Union, Ufaransa, Finland, Ireland, Nertherlands, Norway, United Kigdom  na United States of Amerika. 

Bw. Tutuba alisema TMEA imetekeleza miradi mbalimbali ikiwemo kuwajengea uwezo wataalamu wa Serikali, kujenga baadhi ya vituo vya Pamoja vya forodha mipakani, kununua Scanner inayotumika katika mpaka wa Tunduma, Ukarabati wa Scanner inayotumika Bandari ya Dar es Salaam na wamefanya shughuli mbalimbali za kuhakikisha kwamba nchi inatekeleza Mkakati wa Kitaifa wa kujenga mazingira bora ya kufanyia biashara na kupunguza gharama za uendeshaji wa biashara.

“Tumeongea mafanikio mengi ambayo wameyatekeleza na kwa ujumla tumefahamisha miradi waliyofanya, unajua hawa TMEA wametusaidia katika miradi mbalimbali ya kwenye vipaumbele walivyokuwa wanavitekeleza kwa ujumla kwa sababu vinaendana na mpango wa Maendeleo wa miaka mitano, lakini vilevile wanaendelea kutekeleza dira yetu ya maendeleo ya mwaka 2025 kwa upande wa Tanzania Bara lakini kwa Zanzibar kuna maeneo wamekuwa wakiyafanyia kazi yanayoendana pia na Dira ya Maendeleo ya Zanzibar ya mwaka 2050” Alisema Bw. Tutuba

Aidha Bw.Tutuba alisema wameijulisha Taasisi hiyo kuwa kuna umuhimu wa kuendelea kushirikiana, na kwa wafadhili wote wanaochangia zile fedha wamewajulisha kwamba watazitumia vizuri. Pia Bw. Tututba alimkaribisha Mtendaji huyo mpya wa Taasihi hiyo Bw. David Beer na kumhakikishia kwamba Serikali inayoongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaendelea kutoa ushirikiano kwa wadau wa maendeleo na kwamba Serikali iko mstari wa mbele kujenga mazingira wezeshi ya kuhakikisha shughuli zote za biashara zinafanyika vizuri.

“Tumewajulisha kwamba nchi yetu iko vizuri kiuchumi, kisiasa na hata shughuli mbalimbali za uwekezaji na kufanya gharama za uwekezaji kuwa chini maana yake wawekezaji wengi tunawakaribisha waje kuwekeza nchini na wakati huo huo sisi tunaendeleza kuimarisha miundombinu ambayo itawezesha utekelezaji wa shughuli zao vizuri” alisema Tutuba.

Bw. Tutuba aliongeza kuwa katika majadiliano ya kuandaa awamu ya tatu ya mkakati wa utekelezaji wa pamoja ni kuweka nguvu kwenye miradi mikubwa na miradi mingine midogo midogo iliyokuwa inafanyika na kuangalia pale ilipofanikiwa iunganishwe na kufanya mambo makubwa zaidi lakini pale ambapo bado kuna kuzitatua haraka changamoto  zilizojitokeza.

“Kuhusu usawa wa kijinsia katika uongozi nikiwafahamisha kwamba sasa hivi ukiangalia Tanzania ni nchi pekee ambayo mihimili miwili inaongozwa na wanawake ikiwepo Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu lakini pia tunae Mhe. Dkt. Tulia Ackson Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ni nchi pekee ambayo iko imara na imethibitisha kwamba wanawake wanaweza kuongoza vizuri na nimewataka waangalie namna ya kuwezesha shughuli za kibiashara kwa wanawake na vijana katika vipaumbele vya awamu inayokuja” alisema Tutuba.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu mpya wa TMEA Bw. David alisema ameanza majukumu yake hivi karibuni na Tanzania ni nchi yake ya kwanza kutembelea.

“Najivunia kuwa mwanafamilia wa Trade Mark na tuna historia ndefu na Serikali ya Tanzania hivyo tutaboresha biashara na kuvuka mipaka hasa kusafirisha bidhaa nje. Namshukuru Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Tutuba kwa kuchukua muda wake kuonana na uongozi wa Trade Mark kujadili sio tu mafanikio tuliyoyapata huko nyuma ni pamoja na ufanyaji kazi mzuri wa bandari ya Dar es Salaam na uwekaji wa kituo cha Pamoja Tunduma” alisema Bw. Beer.

Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa TMEA aliyemaliza muda wake Bw. Frank alisema anaishukuru Tanzania kwa ushikiano waliouonesha kwa kipindi cha miaka kumi na mbili ambayo tumefanya kazi pamoja kwani tumefanikiwa vya kutosha.

”Namtakia heri mrithi wangu; Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Tutuba asante sana maana kwa maneno mazuri uliyosema, unayo timu nzuri ambayo itafanya vizuri huko mbeleni “alisema Bw. Frank

Trade Mark ni Shirika ambalo lilianzishwa mwaka 2010 na Makao makuu yake yako Nairobi Kenya ambapo ofisi zake kwa Tanzania ziko Arusha na Dar es Salaam. Kwa sasa TMEA inaendelea kupanua shughuli zake nje ya  Afrika Mashariki.

MWISHO