Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2024/2025
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

HAZINA HUTOA PENSHENI KWA WASTAAFU WASIOCHANGIA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII

02 Jul, 2024
HAZINA HUTOA PENSHENI KWA WASTAAFU WASIOCHANGIA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII

Afisa Hesabu Mkuu kutoka Kitengo cha Pensheni Wizara ya Fedha, Bi. Joyce Chacky (katikati), akitoa maelezo kwa Mstaafu Mzee Rashidi Mbwego, kuhusu aina ya mafao yanayolipwa na Hazina, alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha katıka Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere Barabara ya Kilwa Temeke, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Afisa Kumbukumbu wa Kitengo hicho, Bi. Neema Nyipamato.

 

Ofisi ya Pensheni ya Hazina iliyo chini ya Idara ya Mhasibu Mkuu wa Serikali inajukumu la kulipa mafao ya kustaafu kwa viongozi wa kitaifa na kisiasa na watumishi wa umma ambao hawachangii katika mfuko wowote wa hifadhi ya jamii.

Hayo yamebainishwa na Afisa Hesabu Mkuu kutoka Kitengo cha Pensheni Wizara ya Fedha, Bi. Joyce Chacky, wakati wa Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere Barabara ya Kilwa, Temeke, jijini Dar es Salaam.

Bi. Chacky alisema kuwa aina ya mafao ambayo hutolewa na Hazina kwa mstaafu ni pamoja na kiinua mgongo kwa mtumishi anapostaafu kwa mujibu wa Sheria akiwa na miaka 60 au akistaafu kwa hiari akiwa na miaka kuanzia 55.

Alisema aina nyingine ya mafao ni pensheni ya kila mwezi anayolipwa mstaafu baada ya kustaafu kwa mujibu wa Sheria Sura 371 ya mwaka 1956 na Sheria Na. 2 ya mwaka 2018 ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma.

Bi. Chacky alitaja mafao mengine yanayolipwa na Kitengo hicho kuwa ni pamoja na Mafao ya Mirathi, Pensheni ya kifo, mafao kwa wategemezi, kiinua mgongo kinachotokana na ajali kazini, pensheni ya ulemavu na mafao ya mkataba.

Aidha aliwataka wananchi kutembelea Banda la Wizara ya Fedha ili kupata elimu kuhusu Pesheni inayolipwa na Hazina ili kupata uelewa na pia kuepukana na taarifa zisizo za kweli zenye lengo la kupotosha.

Mwisho.